KAPOMBE BADO, DAKTARI AMUONGEZEA WIKI NYINGINE MBILI ZA MATIBABU


Huku mashabiki wa Simba wakiwa wana hamu kubwa ya kumuona uwanjani, daktari amemuongezea wiki mbili nyingine za matibabu beki Shomari Kapombe.

Kapombe alitarajia kurejea mazoezini wiki hii, lakini daktari ametaka uhakika wa mambo na kumuongezea wiki mbili ili awe vizuri zaidi.

"Hataanza mazoezi, ana wiki mbili nyingine. Daktari anataka kuona tatizo lake la nyonga linaisha kabisa," alisema mmoja wa viongozi wa Simba.

Kapombe amerejea Simba akitokea Azam FC ambayo alijiunga nayo akitokea AS Cannes ya Ufaransa.

Kabla ya hapo, Kapombe alitengeneza jina lake akiwa Simba kabla ya kuamua kwenda kucheza soka la kulipwa nchini Ufaransa.

Maoni