LEMAR 'WA ARSENAL', AIPIGIA MBILI UFARANSA YAILAZA 4-0 UHOLANZI

Mshambuliaji wa Monaco, Thomas Lemar anayetakiwa na Arsenal akishangilia baada ya kuifungia timu yake ya taifa, Ufaransa mabao mawili dakika za 73 na 88 katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Uholanzi usiku wa jana kwenye mchezo wa Kundi A kufuzu Kombe la Dunia. Mabao mengine ya Ufaransa yalifungwa na Antoine Griezmann dakika ya 14 na Kylian Mbappe dakika ya 90 na ushei 

Maoni