Bale arejea uwanjani leo

Wakati Karim Benzema na Cristiano Ronaldo wakiwa wameshindwa kufikia makali yao katika msimu huu 2017/18, kocha wa Real anataka kumtumia Bale katika mchezo dhidi Fuenlabrada katika Kombe la Mfalme.
Madrid, Hispania. Mshambuliaji Gareth Bale amerejea kikosini baada ya kupona majeruhi yake na tayari kocha Real Madrid, Zinedine Zidane amesema anataka kuona BBC ikiongoza safu yake ya ushambuliaji.
Wakati Karim Benzema na Cristiano Ronaldo wakiwa wameshindwa kufikia makali yao katika msimu huu 2017/18, kocha wa Real anataka kumtumia Bale katika mchezo dhidi Fuenlabrada katika Kombe la Mfalme.
"Hatuwezi kucheza na wachezaji 12 au 13," Zidane aliwambia wanahabari.
"Lakini nataka kuwaona watatu hao, Cristiano, Bale na Benzema wakicheza pamoja, kwa sababu sijawaona wakicheza pamoja kwa muda mrefu.
"[Bale] atakuwa na sisi leo. Lengo ni kumuona akicheza dhidi ya Fuenlabrada. Nataka kumuona Bale akiwa fiti kwa asilimia mia moja haraka iwezekanavyo, lakini siwezi kusema wakati akiwa jukwaani.

Maoni