BOCCO MCHEZAJI BORA VPL MWEZI JUNUARI.

Nahodha wa timu ya Simba ya John Bocco amechaguliwa kuwa mchezaji Bora wa mwezi Januari wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL).
Bocco amemshinda nyota mwenzake wa Simba Emmanuel Okwi na nyota wa Mwadui Awesu Awesu.
Bocco ameisaidia Simba kupata pointi tisa mwezi Januari huku akifunga mabao matatu na kutoa pasi mbili za mabao.
Kiwango cha mshambuliaji huyo aliyecheza dakika zote 270 za michezo mitatu ya Simba mwezi huo kilikuwa juu karibu kila mchezo.
Kwa upande wa Okwi aliyecheza dakika 206 kati ya 270 ilizocheza timu yake, alitoa mchango mkubwa kwa Simba kupata idadi hiyo ya pointi na kuendelea kubaki kileleni mwa msimamo wa ligi.
Awesu aliingia katika hatua hiyo kutokana na kung’ara katika michezo ambayo Mwadui ilicheza mwezi huo, akiibuka mchezaji bora katika mchezo wao dhidi ya Yanga katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Kutokana na ushindi huo Bocco atazawadiwa tuzo, kisimbuzi cha Azam TV na fedha taslimu sh. milioni moja kutoka kwa mdhamini mkuu wa ligi kampuni ya Vodacom Tanzania.

Maoni