KWA MKONGO QUEENS YAJITIA KITANZI YAKUBALI KICHAPO CHA MABAO TATU.

Kwa Mkongo imeendelea kujiweka katika mazingira magumu baada ya kukubali kichapo cha mabao matatu kwa bila kutoka kwa Dovya B katika mchezo ambao umefanya leo Jumapili kwenye uwanja wa Dovya B,Dar Es Salaam.

Mchezo ulianza kwa Kasi timu zote zikionekana kutafuta bao la mapema.

Hadi mapumziko Dovya B 2-0 Kwa Mkongo,Kipindi cha pili timu zote zilirejea zikiwa zimejipanga upya lakini Dovya B walionekana kujipanga zaidi,walionekana kuumiliki mchezo kwa asilimia zote na kufanikiwa kupata bao la 3.

Mpaka dakika 90 zinakamilika Dovya B 3-0 Kwa Mkongo.

Kufuatia matokeo hayo Kwa Mkongo wanashika mkia mwa kundi B wakiwa awana alama ata moja na wamesha poteza michezo 4 na wamebakiwa na mchezo moja dhidi ya Mzambarauni ambao nao leo wamekubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Msufini na Matokeo mengine Saku 0-6 Dovya B. 

Maoni