DKT. NDUGULILE AGAWA MIKOPO KWA WAJASIRIAMALI WA WILAYA YA KIGAMBONI.

Mbunge wa Kigamboni Dkt Faustine Ndugulile (Mb) jana Jumatano amegawa mikopo ya Tsh 130 millioni kwa vikundi vya wanawake, vijana na walemavu vya Wilaya ya Kigamboni katika sherehe iliyofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Kigamboni.

Dkt Ndugulile aliipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni kwa kutenga na kutoa mikopo kwa wajasiriamali. 

Hadi sasa halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni imeshatoa mikopo ya Tsh 1.25 Billioni tangu kuanzishwa kwake miaka 4 iliyopita.
Dkt Ndugulile aliwataka waliopewa mikopo kutumia fedha hizo kwa malengo yaliyokusudiwa na kurejesha fedha hizo kwa wakati.

Dkt Ndugulile aliwapongeza maofisa Maendeleo ya Jamii kwa kazi nzuri ya uhamasishaji na kusimamia vikundi hivyo. 
Aidha, aliwataka kuiga mfano wa Ludewa ambako vikundi vya wajasiriamali vimewezeshwa kupata kandarasi mbali mbali za barabara kupitia TARURA.

Imetolewa na:
*Ofisi ya Mbunge wa Kigamboni*
#Kigambonimpya
#Kigamboni
#Ndugulile

Maoni