APR YAMSAJILI MCHEZAJI ALIYEGOMA KUCHEZA BURE HISPANIA

Na Canisius Kagabo, KIGALI
KLABU ya APR FC ya Rwanda, imemsajili beki chipukizi wa kulia Ombalenga Fitina (pichani kushoto)baada ya mipango yake ya kucheza Hispania kugonga besela.
Fitina alikaribia kujiunga na klabu ya Ligi Daraja la Kwanza Hispania, Universidad Catolica de Murcia (UCAM Murcia) baada ya kufuzu majaribio yeye pamoja na chipukizi mwenzake wa Rwanda, Kalisa Rashid.
Lakini wote akaamua kurudi nyumbani, baada ya kuambiwa anapaswa kwanza kucheza kikosi cha vijana cha timu hiyo kwa miezi sita kama mchezaji wa ridhaa, kabla ya kupewa mkatava rasmi, ingawa mwenzake Kalisa Rashid bado hajasaini timu yeyote.

Maoni