BARAKA DA PRINCE ANYANG'ANYWA AKAUNT YA YOUTUBE NA ROCKSTAR400

Muimbaji huyo ametangaza kufungua akaunti mpya ya You Tube na kuiacha ile ambayo aliyokuwa akiitumia akiwa katika label yake ya zamani

Baraka ametoa taarifa kwamba soon atafungua akaunt mpya ya YouTube ambapo kazi zake mpya za muziki zitakuwa zikipatikana kupitia channel hiyo.

Baraka " Ndugu zangu nitawatangazia soon You Tube channel yangu mpya kuna zawadi zenu kama 5 hivi.....basi na hii itadondoka ndugu zangu" aliandika baraka Instagram

Label ya RockStar4000 haijawahi kuzungumza chochote toka muimbaji huyo atangaze kun'gatuka kwa madai kuwa kuna baadhi ya vitu anaona haviendi sawa.

Katika hatua nyingne muimbaji huyo ameonekana kuwa katika maandalizi ya kuachia kazi yake  ya kwanza akiwa nje na label hiyo baada ya kuonekana akiwa location akishoot video ya wimbo wake mpya.

Maoni