Baraza la habari Tanzania (MCT) jana limezindua ripoti mbili juu ya hali ya uhuru wa habari pamoja na

Baraza la habari Tanzania (MCT) jana limezindua ripoti mbili juu ya hali ya uhuru wa habari pamoja na tukio la uvamizi wa kituo cha clouds media.
Akizungumza jijini Dar es salaam, katibu mkuu wa MCT Kajubi Mukajanga amesema tafiti hizo zinafanywa kama inavyolelekezwa na katiba ya baraza hilo. Na kueleza kuwa ripoti hizo zinalenga kuangalia hali ya vyombo vya habari kwa mwaka uliopita kwa maana ya hali ya kiuchumi, sheria, usimamizi, mafanikio pamoja na changamoto.
Kuhusu sakata la Clouds, amesema lengo la utafiti wa tukio hilo ni kutaka kujua kama lilisababisha athari juu ya uhuru wa habari pamoja na uhuru wa uhariri.

Maoni