BAYERN YAUANZA MSIMU MPYA WA BUNDESLIGA KIBABE,YAITUNGUA LEVERKUSEN 3-1 NYUMBANI,VAR YATUMIKA KWA MARA YA KWANZA


Munich,Ujerumani.

MABINGWA Bayern Munich wameuanza vyema msimu mpya wa 2017/18 baada ya jana Ijumaa usiku wakiwa nyumbani Allianz Arena kuitungua timu ngumu ya Bayer Leverkusen kwa jumla ya mabao 3-1.

Mlinzi mpya Niklas Süle ndiye aliyekuwa wa kwanza kuamsha shangwe Allianz Arena baada ya kuifungia Bayern Munich bao la kuongoza katika dakika ya 9 ya mchezo kwa kichwa.


Mabao mengine ya washindi yamefungwa na Corentin Tolisso aliyefunga bao la pili katika dakika ya 19 huku bao la tatu likifungwa katika dakika ya 52 na Robert Lewandowski aliyefunga kwa mkwaju wa penati.

Bao pekee la Bayer Leverkusen limefungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Uswis,Admir Mehmedi katika dakika ya 65 ya mchezo huo ulioshuhudia mvua kubwa ikinyesha dimbani Allianz Arena.

Teknolojia ya VAR yatumika

Aidha katika mchezo huo imeshuhudiwa kwa mara ya kwanza Teknolojia ya VAR (Video Assistant Referee) ikianza kutumika kwenye ligi ya Bundesliga.

Maoni