Campbell aipa Tanzania mbinu za ushindi wa soka

Nyota wa zamani wa klabu ya arsenal Sol Campbell amesisitiza kuwa ili Tanzania iweze kufanikiwa katika soka unapaswa kuwa na falsafa ambayo itaiongoza nchi katika kuendeleza michezo wa mpira wa miguu,Campbell ambaye aliwasili nchini jana akitokea Uingereza amesema hayo leo akizungumza na EATV na kwamba ni vigumu kwa Tanzania kufanikiwa endapo hakutawekwa misingi thabiti na kuisimamia .
Campbell akiwa kwenye mahojiano na mtangazaji wa EATV.
Beki huyo ambaye alikuwemo kwenye kikosi cha Arsenal kilichotwaa ubingwa wa 2003/04 bila kufungwa mechi hata moja na amesema hata taifa lao la Uingereza limetambua hilo na hivyo wanalifanyia kazi ili timu yao ifanye vyema katika mashindano makubwa duniani.
Campbell ni balozi wa Arsenal ambayo inamahusiano mazuri na kampuni ya kubashiri michezoya sportpesa .
Campbell yupo nchini na Leo ataungana na washabiki wa soka kushuhudia mechi ya ngao ya hisani kati ya Arsenal na Chelsea itakayopigwa huko Wembley.

Maoni