CHELSEA YAMSAJILI MDOGO WA EDEN HAZARD


Mabingwa wa England Chelsea imekamilisha usajili wa Kylian Hazard ambaye ni mdogo wa Eden Hazard akitokea klabu ya Ujpest ya Hungary.

Kylian Hazard anakua mchezaji wa tatu kutoka ukoo wa kina Hazard kusaini Chelsea baada ya Eden Hazard na Thorgan Hazard ambaye alitimkia Borrussia Monchendglabach ya Ujerumani.

Mchezaji huyu mwenye miaka 22 anacheza kama kiungo mshambuliaji na ataanzia kikosi cha akiba cha Chelsea kuangalia maendeleo yake kama atafanya vyema atapandishwa kikosi cha kocha Antonio Conte.

Maoni