CHIRWA SASA SAFI, AANZA MAZOEZI NA YANGA TAYARI KWA KAZI




Baada ya kumaliza kujieleza katika kamati ya nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), mshambuliaji Obrey Chirwa anatarajia kuanza mazoezi leo.

Chirwa anarejea katika kikosi cha Yanga baada ya muda wa zaidi ya wiki mbili za kuwa majeruhi.

Raia huyo wa Zambia alikuwa aanze mazoezi jana lakini ilishindikana kwa kuwa alitakiwa kujieleza katika kamati ya nidhamu kwa tuhuma za kumsukuma mwamuzi.

Maoni