Hakuna wa kuziba nafasi yangu- Ruby

Msanii anayefanya vizuri na wimbo wake 'Na Yule' Ruby amesema hakuna wa kuziba nafasi yake katika 'industry' ya muziki huku akidai hawezi kumchukia Nandy kwa kuwa ameshafanya naye kazi nyingi na mafanikio yake ndiyo furaha kwake,Ruby amefunguka hayo kupitia kipindi cha Friday Night Live (FNL) kinachorushwa na East Africa Television na East Africa Radio, baada ya kuwepo kwa tetesi zinazodai kuwa msanii huyo amepotezwa Nandy kwenye muziki.
"Ni maneno ya watu ambayo yapo kila kukicha na mimi siwezi kujifananisha naye kwa kuwa mimi ni Ruby na yeye ni Nandy. Nafasi yangu ipo pale pale", amesema Ruby.
Kwa upande mwingine, Ruby ameweza kuyaweka mahusiano yake wazo kwa mara ya kwanza ndani ya FNL ambapo amelimtambulisha kijana mwenye jina la Genely Hb kuwa ndiye mpenzi wake wa sasa.

Maoni