HII NDIO HALI INAYO ENDELEA NCHIN KENYA.

Polisi wa kukabiliana na ghasia wamekabiliana na vijana waliokuwa wameandamana na kufunga barabara katika mtaa wa Kondele mjini Kisumu.
Maeneo mengine ya mji huo ambao ni ngome ya mgombea wa upinzani Raila Odinga hawakuwa na watu wengi huku biashara nyingi zikifungwa.
Emmanuel Igunza anasema polisi walifyatua risasi halisi hewani kujaribu kuwatawanya waandamanaji.
Maafisa wameingia pia katika baadhi ya mitaa kushika doria.

Maoni