HII NI STORY YA KWELI SOMA UJIFUNZE KITU.....

Nilienda kumzika ibilisi wangu!Ilikuwa
ni ajali kubwa na hata mimi sijui niliweza vipi kupona.Dereva na mke wangu walifia pale pale kwenye eneo la tukio.Tulikuwa tukitokea Chalinze kurudi Dar baada ya kukagua shamba ambalo ilikuwa tulinunue katika kijiji cha Msata
wilayani Bagamoyo.Mbele kidogo ya mji wa Chalinze ndipo ajali hiyo ilipotokea.Dereva wetu
alikuwa akijaribu kulipita lori fulani lakini wakati huo huo gurudumu la mbele la gari letu lilipasuka na kusababisha gari kuyumba ambapo lililivaa lile lori.
Kufuatia kuligonga huko,gari letu lilirudishwa katikati ya barabara ambapo liligongana uso kwa uso na gari lingine lililokuwa linakuja mbele yetu.
Sikujua kilichotokea hadi baada ya siku mbili Muhimbili.Nilipopata fahamu ilinichukua muda kukumbuka
kidogo kilichotokea.Nilipouliza kuhusu mke wangu hakuna aliyesema kitu kati ya wale ndugu na jamaa
zangu waliokuwa pale kando ya kitanda changu.
Pamoja na maumivu yangu nilijua kilichokuwa kimetokea.Nilianza kulia hata kabla hawajaniambia chochote.Kaka yangu aliponiambia “jikaze ni kazi
ya Mungu,shemeji mama Rehema ametutoka.”
Nilipoteza fahamu.Nilipopata fahamu na kukubali kuipokea taarifa ile,niliambiwa kuwa mke wangu alifia pale pale kwenye eneo la ajali pamoja na dereva.
Mimi nilikuwa nimevunjika mguu wa kushoto,mkono wa kushoto na mbavu mbili na kubanwa kifuani. Hali yangu kwa kweli haikuwa nzuri lakini nililazimika kujikaza.Mke wangu alikuwa amekufa,
haikuwa rahisi kukubali.Nilikuwa nampenda na yeye pia alikuwa
ananipenda.Ukweli ni kwamba tulikuwa
tukiaminiana sana na mke wangu ambaye
nitamwita Sia{Jina linalokaribiana na jina lake halisi}.
Tulikuwa tumeshibana kiasi kwamba, kulikuwa hakuna ambaye alikuwa hajui. Nilikumbuka kwamba kwa
miaka minane ya ndoa yetu tulikuwa hatujawahi kukorofishana,ukiacha kusigishana kwa hapa na pale.Nilikuwa sijawahi kumsaliti na hata yeye pia.
Nilijaribu kukumbuka ahadi zetu kwa kila mmoja na kuhusu watoto wetu wawili mmoja wa kiume na
mwingine wa kike.Kwa kweli ilinichukuwa muda wa saa kadhaa kukubali kwamba nilikuwa sina mke,mwili wa yule nimpendaye ulikuwa ukiganda
mochwari.Nilijikuta nikiinuka kwa nguvu na kupiga yowe nikitaka kwenda kumfufua mke wangu.
Nilikuwa nimechanganyikiwa kwa kweli! Ndugu zangu na jamaa waliokuwepo pale wodini walinishika na kunituliza.Ilibidi waombe msaada kwa madaktari ambapo
nilichomwa sindano iliyonipa utulivu na usingizi.
Nilipoamka jioni sana ,nilikuwa na utulivu kidogo,
kaka yangu aliniomba nijikaze na kumrudia mungu.
Aliniambia nijaribu kuukubali ukweli na hali halisi.
Nilijikaza na aliniambia kwamba mazishi ya mke wangu ingebidi yafanyike kesho,kwa mujibu wa makubaliano ya ndugu wa pande zote.Aliniambia
dereva wangu alikuwa amezikwa tayari na ndugu zake.Nilimwomba kaka wauache mwili wa mke wangu ili niwe nae karibu kwa muda fulani.Kaka alinishawishi sana nikubali kwa sababu,kama
muislamu ninajua inavyokatazwa kuuweka mwili wa marehemu bila kuuzika kwa muda mrefu,bila
sababu.Hatimaye nilikubaliana naye,lakini nilisema ni lazima
nami niende kuzika.Kaka alinimbia kwa hali yangu nisingeruhusiwa na madaktari na wala nisingeweza kumudu kwenda makaburini Kinondoni.
Nilimwambia kaka katika yote ningemkubalia lakini sio hilo la kutomzika mke wangu.Nilimwambia,
habari ya madaktari aachane nayo na kuhusu mimi kumudu ningemudu tu. Nilikataa katakata hata kusikiliza ilibidi kaka aondoke pale bila muafaka.
Walikuja ndugu zangu wengine kunishawishi lakini niligoma kabisa, hadi ikabidi wakubaliane nami.
Lakini walijua ingekuwa ngumu sana kutokana na hali yangu.Kesho yake walikuwa tayari wamepata
ufumbuzi.Walikubaliana na uongozi wa hospitali kwamba nipelekwe makaburini kwa gari la wagonjwa.Ni kweli nilikwenda kuzika.Pamoja na
kuwa waislamu huwa hatutoi heshima za mwisho kwa kuuona mwili wa marehemu, mimi nililazimisha hadi nikaonyeshwa mwili wa mke wangu.Alikuwa
hana alama hata moja usoni kwani alikuwa ameumia
miguuni hadi kifuani.Nilipomwona nilipoteza fahamu…………
Tulimzika mke wangu na nikarudishwa hospitalini.Nilitoka hospitalini baada
ya mwezi mmoja na
kurejea nyumbani.
Nyumba yangu mwenyewe ilinitisha na nilihisi simanzi kubwa kuwa mle ndani.
Watoto wangu walinisikitisha zaidi.Lakini
nilishaamua kuikubali hali halisi.Nilikuwa
nimekubali kuanza upya maisha.Siku ya Tatu tangu kurejea nyumbani niliamua kupangua ili kuvipanga upya
vitu vya marehemu.Nilipanga nguo zake na mapambo mengine ya kike.Halafu ilibidi kupanga vitu vilivyokuwa kwenye droo zake ambazo funguo zake alikuwa nazo mwenyewe marehemu.Kwa
sababu sikuwa najua alipokuwa ameweka funguo za droo zile mbili ilibidi nizivunje moja baada ya nyingine.Droo ya kwanza ilikuwa na barua na karatasi mbali
mbali za mawasiliano na mambo mengine. Hapo nilianza kuzisoma barua.Barua ya kwanza ilikuwa ni kutoka kwa mpenzi wake.Haikuwa ni barua ya
zamani,kwani ilikuwa imetumwa kwake miezi minne
tu kabla ya kifo chake.Ilitumwa na bwana
aliyekuwa ametuuzia ile gari iliyohusika kwenye ajali iliyomuua.
Sehemu ya barua ile ilikuwa imeandikwa: Kuhusu
hilo ni sawa mpenzi wangu.Wewe mwambie nitawauzia kwa mkopo,tena kwa bei rahisi sana.
Lakini hizo fedha utazichukua wewe. Kuhusu
kwenda Harare nitakufahamisha, jaribu kwa upande
wako kumwambia kwamba utakuwa na semina huko April.Najua kufika Aprili tutaelekea huko.
Nataka tuwe mahali huru na salama ili niufaidi mwili wako na wewe uumiliki wangu.
Barua hiyo ilijaa upuuzi mwingi…… Nilipomaliza kuisoma nilihisi kama ninayeota au ambaye nitaugua kichaa Ni kweli huyu jamaa
ndiye aliyetuuzia lile gari iliyochukua maisha ya mke wangu kwa bei ya chini sana.Gari Nissan Pajero kwa
shilingi milioni 7.5 nzuri tu,hata kama imetumika!
Kumbe ulikuwa ni mpango wake na mke wangu wa kuipatia familia yangu gari. Nilienda kupekua barua na hati kadhaa. Niligundua hati ya nyumba kwa
jina la mke wangu.Nyumba hii ilikuwa Kijitonyama.Nilipata barua
nyingine.Hii ilikuwa ni ya bwana wake wa zamani lakini ilikuwa imeandikwa mwaka mmoja tu nyuma,ilikuwa ikimlaumu mke wangu kwamba hakuwa
mkweli Sehemu muhimu katika barua hiyo ilikuwa imeandikwa:Ninajua wazi huyo Rehema ni mwanangu na hata
rafiki yangu Mudy amesema tunafanana sana.kama umeamua kunidanganya ni sawa lakini kumbuka hiyo ni damu yangu.Sitamchukua wala kumdai
lakini kujua ukweli ni muhimu kwangu. Nilipomaliza kusoma barua ile nilishikwa na kizunguzungu.Nilitulia hapo kitandani kwa muda.Halafu niliendelea kupekua kwenye karatasi hizo.
Niliona barua kadhaa na kadi za mapenzi. Kadi mbili zilikuwa zinatoka kwa bosi wake.Barua moja ilikuwa ikitoka Uingereza kwa mtu aliyeitwa P.Hughes.
Huyu ni wazi alikuwa ni mpenzi wa mke
wangu kwa muda mfupi,alipokwenda Uingereza miaka miwili nyuma kwa kozi fupi ya miezi sita.
Barua yake ilikuwa imejaa sifa nyingi, akimsifia mke wangu kwa kuwa na mwili mzuri na kuwa mtaalamu wa
mapenzi na ilisifia shanga zake pia.Nilihisi nikibana kifua na mapigo ya moyo wangu
yalikuwa kama yamesimama.Bila shaka siku ile ndipo yalipoanzia maradhi yangu ya shinikizo la chini la damu,ambayo ninayo hadi sasa.Nilivunja
ile droo ya pili ambayo ilikuwa na picha kadhaa.Zote zilikuwa ni picha za mapenzi. Nilitazama mbili za
kwanza,nikatoka chumbani mle nikiyumba.
Naomba nisiseme sana kuhusu picha hizi, kwa sababu,hata kama mtu sio mke wako,ni
mwanamke unayemfahamu tu ukiona picha zake akiwa kwenye hali kama ile, utatahayari sana.Picha unazoziona
kwenye mikanda ya ibilisi au kwenye mtandao wa inteneti ndizo zilizokuwa pale kwenye droo,zikiwa ni za mke wangu na wanaume watatu tofauti.Yule aliyejifanya kutuuzia gari na nyingine za wanaume wawili ambao sikuweza kuwafahamu.
Baadae mchana baada ya kupata nguvu nilimpigia simu kaka mkubwa wa marehemu na kumwomba apite nyumbani.Huyu ni mtu wa hekima sana na hadi sasa tunaelewana sana.Alipofika nyumbani nilimwomba radhi na kumwonyesha barua na picha
zile.Alizitazama kidogo na kunirudishia, alikaa kwa muda na kusema, “Huyu sio dada yangu niliyekuwa namfahamu mimi,hii ni aibu kubwa sana shemeji.”
Hakuweza kusema chochote baada ya hapo.
Alipoondoka kwa huzuni kubwa nilichukua nguo.zote za mke wangu, barua, picha na vitu vingine vyote ambavyo vingenipa kumbukumbu yake na
kwenda kuvichoma moto.Nilivichomea moto shambani kwangu,Kiwangwa
Bagamoyo na kufukia majivu yake.Tangu siku ile hadi leo sijakanyaga kaburini kwake,watoto wake
wanakwenda na huwa nawahimiza kufanya hivyo.
Yule mkubwa anajua mengi hivi sasa baada ya kusimuliwa na baadhi ya ndugu. Nilimwambia kwamba maneno yale hayana ukweli.Lakini najua
anafahamu kuwa yana ukweli,kwani
kuna siku aliniiuliza,mbona haoni picha za mama yake ukutani.Nilimwambia, zinanitia uchungu zaidi.
Ilibidi niende Afrika Kusini kupima DNA, ili kujua kama yule mtoto mdogo ni wangu kweli.Bahati
nzuri ilionesha kwamba ni wangu kwa
asilimia kubwa sana. Hii ilinipa moyo sana .
Kilichonitokea kimenifanya nisiwe na hamu hata ya kuwa karibu na mwanamke,achilia mbali kuoa. Mtu
ambaye umemuamini kuliko binadamu
mwingine,kumbe ndiye anayefanya uasi usio na
kipimo gizani.Nasema hivi mnapaswa kuwaamini wapenzi au wake zenu. Kilichonitokea mimi ni
bahati mbaya na ninaamini kama marehemu angeendelea
kuishi ni lazima ningekuja kumnasa.

Maoni