Je, kuna madhara kama mtu akikaa muda mrefu bila kufanya mapenzi ?

Ukweli ni kwamba hakuna madhara yoyote ya kiafya ukikaa muda mrefu bila kujamii ana . Hakuna madhara yatakayokutokea kwenye sehemu zako za siri au katika sehemu nyingine ya mwili wako . Mwanaume au mwanamke akianza kujamii ana baada ya kukaa muda mrefu , atapata raha na starehe .
Watu wengine wanasema kwamba kutofanya mapenzi kunasababisha kuwa na chunusi usoni au sehemu za siri , au hata kuchanganyikiwa kiakili . Siyo kweli kwamba hali hizi zinasababishwa kwa kutojamii ana , vyanzo vya hali hizi ni tofauti .
Uwe na uhakika kwamba kutojamii ana ni salama kabisa kwako na huwezi kupata madhara yoyote . Lakini kama tulivyosema awali, kujamii ana kunaweza kukaleta matatizo mengi kama mimba i isiyotarajiwa , magonjwa ya zinaa pamoja na maambukizo ya VVU na UKIMWI .

Maoni