JUX KAFUNGUKA: Kutofanya Birthday party kwa miaka minne…kisa?

Mwimbaji staa kutoka Bongoflevani Juma Jux amefunguka siku ya jana August 30, 2017 kupitia Instagram yake na kueleza sababu iliyomfanya kutofanya Birthday party kwa miaka  minne ikiwa mara ya mwisho kufanya hiyo ni mwaka 2013.

Moja ya sababu aliyodai Jux ni kuwa mapenzini na mwanamke ambaye alikuwa faraja kwenye maisha yake ambapo kila ilipofika siku ya kukumbuka kuzaliwa kwake aliridhika na text zake au kuongea naye hata kwa simu na kumtosha.

“Nakumbuka mara ya mwisho kufanya party ya Birthday yangu ilikuwa 2013, Miaka minne iliyopita. Sikuwahi kufanya party yoyote tena sababu nilikuwa na rafiki, mpenzi na mtu wa karibu kuliko mtu yoyote kwenye maisha yangu. Miaka yote iliyofata nilikuwa na yeye mpaka sasa atuko tena karibu kama mwanzo, Tumebaki kuwa marafiki wa kawaida tu .”

“Uwepo wake tu ulikuwa ni zaidi ya chochote kwenye siku yangu ya kuzaliwa, Kuongea na yeye au txt yake tu ilitosha kukamilisha siku yangu. Ila sasa sidhani kama itakuwa kama mwanzo . Nitafarijika sana kama nitamuona hiyo siku. This time nataka kuparty na watu wangu nani anataka kuparty na mimi katika siku ya birthday yangu ?” – Juma Jux.


Maoni