KASEKE AONDOKA SINGIDA, AREJEA DAR KUJIBU MASWALI YA YANGA, ANAUNGANA NA CHIRWA PALE TFF

Kiungo wa Singida United, Deus Kaseke kesho atarejea kuzungumzia mambo kadhaa kuhusiana na klabu yake ya zamani ya Yanga.

Kaseke ameitwa na Kamati ya Nidhamu ya TFF na ataungana Obrey Chirwa kuzungumzia mchezo wa mwisho wa Yanga katika Ligi Kuu Bara msimu uliopita.

Ulikuwa ni mchezo dhidi ya Mbao FC na Kaseke akiwa Yanga pamoja na Chirwa wanatuhumiwa kumsukuma mwamuzi wa mchezo huo.

Mwingine anayetuhumiwa ni Saimon Msuva ambaye sasa anakipiga Difaa Al Jadid ya Morocco.

Wawili hao watajibu maswali ya Kamati ya Nidhamu kuhusiana na kitendo hicho na majibu yao ndiyo yatakayozaa uamuzi wa kamati hiyo.

Maoni