KISA KICHUYA KITUO CHA KULEA VIPAJI CHA MORO KIDDS KUFUNGWA

Uongozi wa kituo cha kulea vipaji vya soka cha Moro Kids cha mjini Morogoro umesema kwa sasa unakifunga kituo hicho kwa muda ili ufuatilie haki zake zinazotokana na usajili wa wachezaji Aly Shomari na Shiza Kichuya ambao sasa wanaichezea Simba ya Dar es Salaam.

Uongozi huo umesema unajiandaa kupeleka malalamiko yake katika ofisi za shirikisho la soka nchini, TFF kutokana na taratibu za usajili kuhusu haki zao kama kituo kilichowalea wachezaji hao kukiukwa.

Inadaiwa na Moro Kids kwamba wao walimtoa mchezaji Ali Shomari kwenda Mtibwa Sugar kwa mkopo, lakini wanashangaa kuona mchezaji huyo anesajiliwa na Simba bila wao kuhusishwa.

Kuhusu Shiza Kichuya, Moro Kids wanadai 15% ya fedha za usajili wake kama ambayo zilivyo taratibu za wachezaji waliolelewa katika vituo.

Maoni