Kiungo wa Sony Sugar aitwa Taifa Stars, Kuwavaa Botswana.

Kiungo wa Timu ya Soka ya Sony Sugar ya Migori nchini Kenya Abdallah Hamisi, ameitwa katika kikosi cha Timu ya Taifa ya Soka ya Tanzania 'Taifa Stars'.

Abdallah anaungana na wachezaji wakongwe kama Salim Mbonde, Erasto Nyoni na Kelvin Yondani kuitumikia Timu ya Taifa katika michezo ya Kirafiki itakayofanyika Septemba mwaka huu.

Kikosi kamili Kilichoitwa Leo na kocha Salumu Shabani Mayanga ni pamoja na:

Makipa.

Aishi Manula, Mwadini Ally na Ramadhan Kabwili.

Mabeki.

Boniface Maganga, Abdi Banda anayekipiga Baroka FC ya Afrika Kusini, Gadiel Michael, Mkongwe Kelvin Yondani, Salim Mbonde na Erasto Nyoni.

Viungo.

Ni pamoja na Himid Mao, Mzamiru Yassin, Said Ndemla, Simon Msuva, Shizya Kichuya, Farida Musa na Morel Ergenes ambaye anaitwa kwa Mara ya pili katika Timu hiyo.

Washambuliaji.

Raphael Daudi, Kelvin Sabato, Mbwana Samatta na Elius Maguri.

Kikosi hicho kitajaandaa na michezo miwili ya Kirafiki na timu ya Taifa ya Soka ya Botswana Septemba 2, Mwaka huu katika Mchezo utakaopigwa kwenye uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam pamoja na mchezo mwingine Septemba 5, ambao bado haujapatiwa timu.

Timu hiyo itaingia kambini Mapema kesho jioni kujiandaa na michezo hiyo.

Maoni