Mahrez arudi nchini Uingereza kukamilisha usajili, haya mengine pia yanaweza kutokea kabla ya usiku wa leo

Ryad Mahrez ameondoka katika kambi ya timu ya taifa ya Algeria hapo jana usiku na kurejea nchini Uingereza kukamilisha masuala yake ya usajili, Mahrez haijafahamika ni klabu gani anakwenda kukamilisha usajili lakini leo inaweza kufahamika.

Uwanja wa mazoezi wa St Georges Park hii leo utakuwa uko busy kumsainisha Oxlade Chamberlain na mashabiki wengi wa Liverpool watakusanyika karibia na uwanja huo ili kuone nyota huyo aliyewatosa Chelsea na kujiunga nao kwa ada ya £40m atapewa jezi namba ngapi.

Haijafahamika mara moja kama Liverpool wanaweza kumchukua Thomas Lemar hii leo au laa, Liva walikuwa na £70m ofa ambayo ilionekana kuwavutia Monaco lakini inasemekana leo katika siku ya mwisho ya usajili Monaco wamepandisha dau hadi £100m.

Baada ya kuitosa Manchester United akaja akaitosa Chelsea sasa kinda wa Ureno ambaye anaichezea Bayern Munich Renato Sanchez imethibitika kwamba anaelekea Swansea, lakini Sanchez anaenda Swansea kwa mkopo huku mkataba wake ukiwa hauna kipengele cha kumuuza.

Manchester City wameamua kumkomalia Alexis Sanchez katika siku ya mwisho ya usajili, City wanajaribu kwa kila namna kumaliza kesi ya Sanchez kabla ya usiku wa leo lakini Arsenal nao inadaiwa wako tayari kumtoa Sanchez endapo tu watampata Thomas Lemar.

Mawakili wa Chelsea wamekutana na Athletico Madrid kwa ajili ya kukamilisha dili la Diego Costa na inasemekana kwamba pande zote mbili zimefikia pazuri kuhusu dili hilo, Diego Costa anaweza kwenda Everton kwanza wakati akisubiri kujiunga rasmi na Athletico.

Maoni