MAMBO 10 YA KUFANYA UNAPOKUWA KATIKA HALI YA KUKATA TAMAA

‘’Nimekata tamaa sidhani kama nitafanya hiki kitu’’ Kila mtu amewahi kusema hivi katika moja ya njia zake katika maisha. Lakini kabla hujaanza kujisemea mabaya . sema haya mambo 10 ili upate nguvu ya kumalizia yasiowezekana .
1.Hii ni changamoto kwa ajili yako
Ni sawa kukubali kuwa kitu hicho ni kigumu, Hutakiwi kuwa katika hali ya kukataa, kubali changamoto  na kufanya uamuzi wa kukabiliana kwa ujasiri na kwa uwezo wako wote.
2.Uwe na Shukrani.
Jaribu kuandika angalau mambo kadhaa ambayo tayari unaona unayo wakati unapokuwa unapita katika ugumu wa mambo yaliopo wakati huo. Pata muda wa kuangalia mazuri katika maisha yako .
3.Pata muda wa kupumzika.
Inuka, pumua kwa nguvu na tembea . hata kuondoka katika mahali ambapo ndipo penye tatizo, itakusaidia kurudisha akili yako kutambua na kuelewa kazi iliopo kuwa ni ngumu. Na utaweza kupata mbinu za kukabiliana nacho.
4.Kuomba Msaada sio Kuonekana Kushindwa
Kuomba msaada sio dalili ya udhaifu ;ni dalili ya ubinadamu . usiogope kuomba msaada unapohitaji kufanya hivyo.. Watu wanaokupenda wanataka kukusaidia hata hivyo.
5.Unafanya hivi kwa Sababu.
Kumbuka kwa nini umeanza. Huenda ni kazi au biashara au chochote ulichoanzisha . haijalishi kuna kazi ya namna gani jikumbushe kwa nini unahitaji kufuata . Kukumbuka kusudi lako itakufanya upate nguvu ya kusonga mbele.
6.Unaweza kufanya mambo magumu.
Kitu unachokiendea ni kigumu sana ,Lakini utaweza kufanya.Mara nyingi vitu huwa na changamoto nyingi unapoona ugumu wake. Jikumbushe kuwa Hakuna kisichowezekana . Hata kama unajisikia kuwa haiwezekani.
7.Umewahi kupita Mambo Magumu Kabla.
Unaweza kumaliza kazi hio ngumu , kwa sababu umeshakumbana na mambo mengine magumu kuliko hayo. Nina uhakika utaweza.
8.Hapa Kuna mbinu
Weka hicho kitu katika kazi ndogo ili uweze kukamilisha. Kama lengo lako lilikuwa ni Kuweka Duka kubwa liwe na kila kitu ndani, na unaona kama kuchanganyikiwa. Jaribu kugawanya hivyo vitu kila kitu na aina yake , kisha weka watu wakusaidie., Kufanya vitu vyote kwa wakati mmoja unaweza kuzidiwa. Lakini kama ukigawanya  utapata nguvu ya kuendelea. Fanya kila kitu kwa wakati wake, hapo ndio utashangaa jinsi utakavyoweza kukamilisha kila kitu .
9.Uwe na ujasiri.
Jaribu kubadilisha pozi lako. Kama ulikuwa unaangalia chini kwa kuona kama umeshindwa, Angalia mbele na usitazame watu, songa mbele na utayaona malengo yako yakifanikiwa .. Mtu mwenye ujasiri huwa haangalii watu wanasema nini au wanafikiri nini juu yake . Anachoangalia yeye kila kitu kiwe kwenye usalama . hasa yeye mwenyewe na malengo yake. .
Hakuna mtu ambaye amewahi kufanikiwa kama anafikiria , anaogopa na kuwa na wasiwasi wa kuwa watu watasema nini , watafikiria nini. Hilo ni kosa kubwa kwenye mafanikio.
10.Achilia mawazo mabaya yaondoke.
Achilia vitu ambavyo vinakushikilia, mawazo mabaya kuhusu wewe mwenyewe, kuchanganyikiwa, woga na vingine utajikuta unaona urahisi wa kuachana na kila kitu kinachokuja mbele yako ambacho hakina maana kwako.
Haijalishi ni changamoto ya aina gani ulionayo. Utaweza. Ulishafanya mambo magumu kabla ya hayo. Unaweza. Wewe ni mshindi.

Maoni