Man City wanaongoza  kuifaidisha Monaco kipesa msimu huu, wenyewe wauza sanaa na kununua kidogo

Baada ya msimu bora kabisa uliopita klabu ya Monaco kufanya vyema katika ligi kuu nchini Ufaransa na ile ya Ulaya, karibia kila klabu kubwa duniani zilianza kutokwa na udenda kwa wachezaji wa Monaco.

Wengi walikuwa hawafahamiki hapo kabla na hata majina yao walikuwa wakizungumziwa tu nchini Ufaransa na sio duniani, lakini baada ya msimu kuisha dunia nzima kwa sasa inawaongelea nyota wa klabh ya Monaco.

Monaco wamepiga pesa sana katika dirisha hili la usajili, mauzo ya takribani £263 wameshahafanga kwa kuwauza nyota wao kwenda klabu mbali mbali huku matajiri wa Uingereza Man City wakiwa ndio wanaongoza kwa kuwapa pesa Monaco.

Man City hadi hivi sasa wameshawapa Monaco kiasi cha £95m kwa kumnunua Benjamin Mendy na Bernardo Silva huku Chelsea wakifuatia kwa kuwapa pesa Monaco baada ya kumnunua Temoue Bakayoko kwa kiasi cha £40m.

Kiujumla hadi sasa Monaco wamekula kiasi cha £263, lakini kama hiyo haitoshi Kylian Mbappe anakaribia kuwapa £166m kama usajili wake kwa mkopo kwenda PSG utafanikiwa kwani baadae PSG watatakiwa kutoa kiasi hicho ili kumpata Mbappe na jumla itawafanya PSG kupata £329.3m huku Lemar naye akiwa njiani.

Pamoja na kuingiza pesa yote hiyo lakini Monaco hadi sasa usajili mkubwa waliofanya ni wa Keita Balde toka Lazio aliyenunuliwa kwa £27m akifuatiwa na Youre Tielemans aliyenunuliwa kwa £21.6m kutoka Anderlchelt.

Monaco wamenunua wachezaji saba huku wengine watatu wakiwapata kwa bure kabisaa na jumla usajili wao umewagharimu kiasi cha £88.9m kiasi ambacho hakifikii hata nusu waliyouza wachezaji wao katika msimh huu.

Maoni