Marekani imeshinda Riadha za Dunia kwa mara yake ya 12 kwa kuzoa medali 10 za.........

Marekani imeshinda Riadha za Dunia kwa mara yake ya 12 kwa kuzoa medali 10 za dhahabu, 11 za fedha na tisa za shaba jijini London nchini Uingereza, Jumapili.
Kenya, ambayo ilikuwa inatetea taji ililoshinda mwaka 2015, ilimaliza katika nafasi ya pili baada ya kuvuna dhahabu kupitia Elijah Manangoi (mita 1500), Hellen Obiri (mita 5000), Conseslus Kipruto (mita 3000 kuruka viunzi na maji), Faith Chepng’etich (mita 1500) na Geoffrey Kirui (marathon).

Maoni