Matumaini ya Wakenya kwa Manangoi na Obiri-Diamond League Uswizi

Matumaini ya Wakenya kwa Manangoi na Obiri-Diamond League Uswizi
Baada ya kumalizika kwa mashindano ya dunia ya riadha ya IAAF jijini London wiki iliyopita, vinara wa mchezo huo kwa sasa wanaelekeza nguvu zao mjini Zurich Uswizi kwa fainali ya msururu wa IAAF diamond league unaofuata mfumo mpya kwa mara ya kwanza tangu uzinduzi wake.
Bingwa wa dunia wa mita 1500 Elijah Manangoi na mshindi wa 4 kule London, Hellen Obiri kutoka Kenya watashiriki mashindano hayo.
Mashindano haya ya siku 4 yataanza kesho katika uwanja maarufu wa Letzigrund, jumla ya wanariadha 18 ambao ni mabingwa watetezi katika mbio tofauti za dunia watakuwa wakilenga kuendeleza ufanisi wao kwa kunyakua ubingwa wa Diamond League.

Maoni