MIMBA SIO UGONJWA: KIKWETE

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Kikwete amesema mimba haipaswi kutazamwa kama ugonjwa na juhudi zinatakiwa kuchukuliwa katika kuhakikisha mama na mtoto hawapotezi uhai wakati wa kujifungua.
Dkt. Kikwete ameitoa kauli hiyo akiwa nchini India akiwa kwenye ziara ya ajifunze namna ambayo taifa hilo limefanikiwa kupunguza vifo vya kinamama wajawazito.
Akizungumza na waandishi wa habari nchini humo, Dkt. Kikwete amesema tukio la kujifungua linapaswa kuwa shangwe miongoni mwa wanafamilia na si huzuni kama ambavyo imekuwa mara nyingine kwenye familia mbalimbali.
Katika ziara hiyo ziara Dkt. Kikwete amekutana na Waziri wa Afya kutoka Jimbo la Rajasthan, Kali Charan Saraf ambaye amemueleza juhudi walizofanya katika kukabiliana na vifo vya kinamama wajawazito.
Dkt. Kikwete anafanya ziara yake nchini India yenye lengo la kujifunza ni kwa namna gani vifo vya kinamama wajawazito pamoja na watoto wenye chini ya umri wa miaka mitano vinadhibitiwa.

Maoni