MIPAZO ARTIST,BIFU ZITO NA MAKONDA WA DALADALA.

Msanii anae chipukia kwa kasi Abduli Mipazo ajikuta anapata wakati mgumu,na kushindwa kabisa kupanda daladala, baada ya kuachia wimbo wake mpya unao kwenda kwa jina la Makonda,wimbo huwo ambao umezungumzia tabia mbaya za baadhi ya makonda wa daladala. Mipazo artist ameyasema ayo kupitia ukurasa wake wa facebook kwa kuandika yafuatayo "Nyimbo Yangu ya makonda
yaniweka mashakani
kwa kile nilichokiimba kuhusu tabia mbaya za baadhi ya makonda wa dala dala jijini
na kunifanya nishindwe kupanda daladala na kutumia usafiri wa boda boda au tax
MAKONDA wengi wamekuwa wakinishutumu na kunipa lawama kwa kile nilichokiimba katika nyimbo yangu
ingawa imepokelewa vizuri na baadhi ya mashabiki zangu"

Maoni