Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amekabidhi

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amekabidhi vifaa vya utendaji kazi katika shirika la Utangazaji Tanzania TBC ikiwemo gari pikipiki tatu na kompyuta.
Akikabidhi vifaa hivyo Makonda amesema kuwa watumishi wa umma wanaunga mkono juhudi zinazofanywa na Shirika la Utangazaji TBC ndio maana akaona tija ya kuleta misaada hiyo.
Kaimu Mkurugenzi wa TBC Martha Swai amesema vifaa hivyo vitaongeza kasi ya utendaji kazi huku Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Matukio Prudence Constatine akiahidi kuendelea kuchapa kazi kwa bidii.

Maoni