MTII MUME WAKO:

Usisubutu kabisa kumpa habari mbaya mume wako km maneno makali akiwa mbali hasa kazini, safarini, ama kwenye mihangaiko yke,
Tafuta mbinu yakumliwaza yakumfariji ili uchofu umuondoke atulie apunzike ndio muongee,
Uongo na usaliti katika ndoa ni sumu ya ndoa npende mumeo kwa dhati km unavyojipenda nafsi yako,
Mthamini na mjali chunga mdomo wako unapozungumza nae uongea kwa upole na unyenyekevu,
Mkaribishe kwa bashasha kila anapoingia ndani usijipambe na kutoka nje jipambe ukiwa ndani kwake,
Usijitie manukato ukatoka nje mtilie ndani akiingia asikie harufu nzuri na sio kukukuta vururu,
Thamani ya mume ni kubwa kwa Allah kwani wake hawawezi kupata pepo bila kuwatii waume zao.
Akina mama tujitahidi kuwathamini waume, kuwatii, na kulinda ndoa zetu.
Allah atupe wepesi tutekeleze mema yalioamrisha ukitenda haya ndio limbwata halisi alilokubali Allah sio kuwaendea kwa waganga waume, kuwaroga ili wewe mwanamke uwe juu mume awe chini
Limbwata ni mapenzi ya dhati sio uganga wala uchawi, elewa iko siku hayo madawa yataisha nguvu utaadhirika mbele yke, na mumeo hapo ndio mwisho wa ndoa yako.
Jamani tuwache ushirikina tenda mema yaliyoamrishwa na Subhanahu Wataala, mtii mumeo ndio penzi linaponawiri na Allah atawalindia na kuwabariki ndoa zenu.
Jitahidi kusambaza ujumbe huu... kwa wanandoa wote in shaa allah,
Na pepo zipo kwenye nyayo za waume zetu.

Maoni