*MUNGU, MAMA 'ANGU* *1*

Na
*Omar Zongo*

Ilikuwa ni furaha kutimiza ndoto yangu ya kuolewa!

sio kila binti rika langu amepata bahati hii kwakweli kwangu ilikuwa ni zaidi ya furaha sasa nilikuwa kwenye gari na mume wangu tukielekea nyumbani kwangu ambapo aliniandalia na akaniambia ni nyumba ambayo tunaenda kuizindua wote.

nilikuwa na shauku yakupaona kwangu, muda mwingi wakati wa uchumba wetu mume wangu aliniambia tukioana tu tunahamia kwetu yaani mimi nitaondoka nyumbani kwetu na yeye ataondoka nyumbani kwake alipokuwa anaishi mwanzo ili tukaanze maisha yetu mapya ya ndoa ndani ya nyumba mpya.

Tuzo alikuwa ni mwanaume niliyekuwa namuomba kwenye maombi yangu kila siku, karibia sifa zote alikuwa anazo!

kwanza alikuwa na mvuto wakiume, urefu wake ulitosha kunifanya mimi nionekane mfupi nikisimama nae pia umbile lake lilijaza baadhi ya maeneo kama kifua nakufanya nijihisi salama muda wote nikitembea nae! kujazia kwake kulinifanya nijione niko na mlinzi wangu kidume kitakachonitetea hata kukitokea tifu.

Pia Tuzo Mume wangu alikuwa mcheshi na wakati mwengine mkimya na roho yake ilitosha kumuona mwema kipindi chote cha miezi sita yakujuana nae kabla ya ndoa.

sifa nyengine kati ya nyingi ambazo nashukuru MUNGU kwakunipa Mume huyu ni kwamba alikuwa mnyenyekevu kwangu licha ya utajiri wa kadiri aliojaaliwa.

tofauti na wanaume wengi wenye pesa ambao wametunukiwa dharau na kiburi hasa wanapobaini kuwa mwanamke anayemuoa hana mbele wala nyuma.

nikiwa kwenye gari aina ya verosa ya mume wangu nilikuwa nawaza maisha mapya ambayo nitaenda kuyaishi na mwanaume huyu ambaye muda wote nilijiapiza kuwa nitakuwa mwema kwake katu sitatia doa ndoa yangu.

"vipi mke wangu...uko sawa?"  sauti hii ya Tuzo mume wangu ndiyo iliyonitoa kwenye wimbi zito la mawazo.

"niko sawa mume wangu, najaribu kuwaza nakumuomba MUNGU aniongoze katika misingi ambayo itakuwa ni furaha na amani kwetu sote.."

nilimjibu hivi mume wangu huku wazi macho yangu yakiniambia kuwa yanavutiwa mno na mwanaume yule ninayemtazama.

nilimshuhudia akitabasamu huku pia nikiona umakini kwenye zoezi lake la kuendesha gari.

"Kuchagua changarawe moja katika nyingi zilizomwagwa ili kukarabati jabari lenye kuaminika ni suala la makubaliano ya wewe mteuaji na changarawe unayoichagua......" alizungumza kwa sauti nzito Tuzo wangu lkn iliniwia ngumu kidogo kung'amua anachomaanisha ingawa baadae kidogo nilianza kumuelewa.

nikweli Tuzo kabla yakunitamkia anataka kunioa alikuwa ni mwingi wakuniuliza maswali kama vile nitakuwa tayari kufuata misingi na taratibu ikiwemo imani yake kuhusu maisha haya kama mume wangu!?

nijuavyo mimi nikawaida ya mke kufuata misingi ya mumewe ili aweze kuishi nae kwa amani na kukiuka ni chanzo cha migogoro hivyo sikuwahi kumkatisha tamaa Tuzo nilimuahidi nitafata anavyopenda  wala sitaenda kinyume.

mara kwa mara alikuwa akinisisitiza suala la mimi kutoenda kinyume nayeye hasa atakaponioa na aliniambia anataka kujenga misingi imara ya familia yetu na vizazi vyetu yaani watoto nitakaozaa nae.

hakika nilikuwa namshukuru MUNGU kwa kunipa mume huyu yaani huwezi amini eti muda tunazungumza mawili matatu kuhusu maisha yetu ndani ya ndoa ghafla akasimamisha gari akaanza kuigiza analia kama mtoto eti alikuwa akipiga miguu chini akisema amesahau nyumba yetu ameijenga wapi.

yaani nyie TUZO kwa masikhara na vituko mwenzenu ndani ya gari nilibaki namuangalia tuu nikitaka kucheka kwa vituko vyake lkn ndani yangu nikijiambiza "nampenda huyu mwanaume"

tukiwa tumesimama eneo lile ghafla niligundua kitu kilichonishtua mno nikabaki mdomo wazi nisiamini ninachokiona......

NI NINI HIKI???

USikose Sehemu ya 2 ya HADITH HII YAKUSISSIMUA!

*MUNGU, MAMA ANGU!*

Na

*Omar Zongo*
tembelea
ommyzongo.blogspot.com
SIMULIZI ZINAISHI.

Maoni