NADHARIA MBALIMBALI KUHUSU HISTORIA YA KISWAHILI

Kiswahili Asili Yake ni Kongo
Baadhi ya wataalamu hudai kuwa asili ya lugha y Kiswahili ni huko Kongo ambayo baadaye iliitwa Zaire na sasa inaitwa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo. Dai hili linaimarishwa na wazo lingine linalodai kwamba katika vipindi kongwe vilivyopata kuwako, sehemu za Pwani ya Afrika mashariki hazikuwa zimekaliwa na watu. Kutokana na hali ya vita, uchungaji na biashara, inadaiwa kuwa Wabantu walitoka sehemu za Kongo walisambaa na kuja pwani ya Afrika mashariki kupitia Kigoma. Baadhi ya wabantu hawa walipitia sehemu za Uganda. Wakati wa kusambaa kwao, walieneza pia lugha zao ikiwem hii ya Kiswahili.
Udhaifu wa nadharia hii ni kwamba, madai ya kuwa asili ya Kiswahili ni Kongo hayana msingi kwani mpaka sasa wataalamu wanaodai hivi hawajaweza kueleza na kuthibitisha kisayansi ama Kihistoria juu ya lini hasa watu walianza kuishi pwani ya Afrika mashariki.
Kiswahili ni Ki-Pijini au ni Ki-Krioli
(i) Kiswahili ni Ki-Pijini
Baadhi ya wataalamu hudai kuwa Kiswahili ni Ki-Pijini. Wataalamu hawa hudai kwamba Ki-Pijini n lugha ambayo huzaliwa kutokana na kukutanika
kwa makundi mawili (A) na (B) yanayotumia lugh mbili tofauti. Ili makundi haya yaweze kuwasilian kunaundwa lugha ambayo kitabia ni tofauti na zile zinazozungumzwa na makundi yanayohusika Lugha hii inaweza kuwa na msamiati mwingi kutoka lugha kati ya zile mbili, au inaweza kuwa na msamiati wenye uzito sawa. Lugha hiyo ndiyo inayoitwa Ki-Pijini. Mazingira yanayosababisha kuwepo Ki-Pijini ni kama vile biashara, utumwa, ukoloni, nk.
Kwa mantiki ya nadharia hii, wataalamu hawa hukiona Kiswahili kuwa kilianza kama Ki-Pijini kwani ni tokeo la mwingiliano baina ya wenyeji w pwani ya Afrika Mashariki na wageni wa kutoka Mashariki ya Kati, hususan Waarabu. Aidha, husisitiza kuwa lugha ya Kiswahili haikuwepo kabla ya hapo.
(ii) Kiswahili ni Ki-Krioli
Wataalamu hawa wanadai kwamba watu wanaozungumza Ki- Pijini wanaweza kuishi pamoja kwa muda wa karne nyingi na kwa hiyo wakaweza kuzoeana na hata kufikia hatua ya kuoana. Wakioana watoto wao huikuta lugha ya ki-Pijini ama lugha yao ya kwanza. Inapofikia hatua ya aina hii kwa watoto wanaozungumza lugha hiyo, wao husemekana sasa
wanazungumza lugha ya Ki-Krioli, lugha ambayo ni hatua ya juu ya Ki-Pijini, yaani Ki-Pijini kilichokomaa.
Nadharia hii hutumia kigezo cha msamiati wa Kiswahili kuonesha uhusiano uliopo kati ya Kiswahili na Kiarabu. Wanadai kuwa, msamiati mwingi wa Kiswahili unatokana na Kiarabu. Hivy huhitimisha kuwa hapana shaka Kiarabu kimehusika katika kuizalisha na kuikomaza lugha ya Kiswahili.
Udhaifu wa nadharia hii ni kwamba hutumia kigezo cha msamiati tu bila kuzingatia vipengele vingine vya lugha kama vile matamshi, maumbo ya maneno au muundo wa sentensi za Kiswahili. Aidha, wataalamu hawa hawakuhoji suala la kufanana kwa Kiswahili na lugha jirani katika hay yaliyotajwa hapo juu na katika eneo la Kijografia ambamo Kiswahili na lugha hizo nyingine hujikut zikizungumzwa. Vigezo hivi ni ushahidi tosha unaoonesha kuwa Kiswahili SI Ki-Pijini wala SI KiKrioli, bali ni lugha kama zilivyo hizo lugha jirani.
Kiswahili ni Lugha ya Jamii ya Vizalia
Kundi la kwanza la wataalamu wa nadharia hii, Bishop Edward Steera, Bwana Taylor, Dkt. R. Reusch, (Katika Maganga, 1997) hudai kwamba:
· Waarabu na Waajemi waliohamia pwani y Afrika ya Mashariki waliwaoa wanawake waAfrika.
· Watoto wao walijifunza maneno ya Kiarab ki-Ajemi kutoka kwa baba zao.
· Aidha, watoto hao wakajifunza maneno yBantu kutoka kwa mama zao.
· Katika jitihada zao, watoto hao walijirekeb kutokana na tamaduni za wazazi wao amba tafauti: utamaduni wa Kiarabu na utamaduni ki-Bantu.
· Vizalia hawa wakaanza kutumia lugha mp mseto wa Kiarabu, Kiajemi na lahaja mbalim za ki-Bantu.
· Kwa kiasi kikubwa, lugha mpya ya mseto ilikuwa ni upotoshaji wa lugha ya Kiarabu na Kiajemi.
· Mwarabu au Mu-Ajemi alikuwa muumini dini ya Uislamu.
· Umo humo, vizalia hawa wakayaingiza ma ya Kiarabu, Kishirazi na Kihindi katika hii lugh mpya.
· Pamoja na kuyaingiza maneno ya kigeni, lugha-mpya yao hii (Kiswahili), ilikithiri vionjo vya lugha mbali mbali za ki-Bantu.
· Ndipo baadaye, lughampya yao hii ikajulik au kuitwa Kiswahili.
· Kwa maoni ya wataalamu hawa, sehemu kati ya tano (2/5) ya maneno yanayotumika k lugha hii mpya ni ya ki-Bantu.
· Sarufi ya lugha mpya hii ni mseto wa ki-B (chenye utata na kisicho na mpangilio maalu pamoja na Kiarabu (chenye mantiki na kilichokomaa).
Kundi la pili la wataalamu wa nadharia hii, B. Krumm na F. Johnson lina mawazo yanayodai kwamba:
· Kiswahili kilitokana na visiwa vya Lamu, Kilamu/Kiamu.
· Wageni kutoka Ghuba ya Ushirazi/Uajemi Arabia ya Kusini walikuja katika Pwani ya Afr ya Mashariki na lugha tofauti.
· Lakini kutokana na kuoana kwao na weny wageni hawa wakaichukua lugha ya hapo walipofikia, wakaikuza kwa maneno kadhaa sentensi kadhaa kutoka lugha zao za asili, ya Kiarabu, Kiajemi na Kihindi hususan katika masuala ya biashara, ubaharia, vyombo vya zao na nguo.
· Aidha, utumwa na tabia ya kuoa wake we ilisaidia kutoa kundi kubwa la masuria. Hali h ikaondosha hisia za ugeni katika lugha zao; n maneno yote yakabatizwa kuwa ya ki-Bantu, hata kupoteza kabisa sura ya ugeni.
Kiswahili ni Kiarabu
Kuna hoja kuu tatu ambazo baadhi ya wananadharia hii huzitumia kutetea nadharia hii kuwa Kiswahili asili yake ni Kiarabu.
(i) Inadaiwa kuwa maneno yenye asili ya yaliyomo katika Kiswahili ni ishara tosha k lugha hii ilianza kama Pijini ya Kiarabu.
(ii) Inahusu neno lenyewe Kiswahili ambalo yake ni Kiarabu. Neno Kiswahili linatokana neno “sahili” (umoja) na “swahil” (wingi) lin maana ya pwani.
(iii) Inadaiwa kwamba kwa kuwa Kiswahili kili pwani, kwa kuwa idadi kubwa sana ya weny pwani ni waislamu, na kwa kuwa uisilamu na Waarabu, basi Kiswahili nacho kililetwa Waarabu.
Kiswahili si Kiarabu
Madai kwamba Kiswahili si Kiarabu yanathibitishwa na hoja kinzani zifuatazo:
Tukianza na dai la kwanza ‘kwamba maneno yenye asili ya Kiarabu yaliyomo katika Kiswahili ishara tosha kwamba lugha hii ilianza kama pijini ya Kiarabu’ tunaona wazi kwamba madai haya hayana mashiko. Lugha ya Kiswahili imetokea kuwa na maneno ya mkopo yenye asili ya Kiarab (na kwa hakika yapo yenye asili ya Kiajemi, Kireno, Kihindi, Kijerumani, Kiingereza nk.) kutokana na ukweli kwamba kulikuwa na mawasiliano ya karne na karne baina ya wenyeji wa pwani na wafanyabiashara wa Kiarabu. Wasemaji wa lugha mbili tofauti wanapokutana hawaachi kuathiriana kilugha. Kwa hiyo lugha kuwa na maneno mengi ya mkopo kutoka lugha nyingine, haifanyi lugha hiyo isemekane kuwa imetokana na hiyo lugha nyingine.
Pili wataalamu hawa wanadai kwamba neno lenyewe Kiswahili lina maana ya Kiarabu .
Kwani linatokana na neno “sahili” (umoja) na “swahil” (wingi) lina maana ya pwani. Hapa ingetupasa tuelewe kwamba kila mtu binafsi au jamii binafsi aghalabu hajiiti mwenyewe jina lake yeye huitwa kwa hilo jina alilopewa na wengine: Jamii yake au wageni waliomtembelea kwake. N hivi ndivyo ilivyojitokeza kwa upande wa jamii ya watu wa pwani ya Afrika mashariki, yaani Waswahili, walipotembelewa na Waarabu na kuitwa As-Sahilyy au As-Sawahiliyy, na nchi yao kuitwa sahil (wingi wake Sawahil), yaani pwani (upwa), ufuo. Kwa mantiki hii, dai hili halina mashiko !
Kigezo cha dini nacho hakikubaliki lugha haiwi lugha kwa sababu ya imani. Hata hivyo lugha ya Kiarabu yenyewe ilikuwepo karne nyingi kabla ya kufunuliwa dini ya Uislamu. Hali kadhalika, lugha nyingine za Kimagharibi zilikuwepo karne nyingi kabla ya kufunuliwa imani ya ukristo. Kama ilivyo kwamba Kiingereza au Kijerumani si ukristo, basi ndivyo vivi hivyo ilivyo kwamba Kiswahili hakiwe kuwa dini ya uislamu, aslan! Wala Kiarabu nacho si uislamu. Tunachoweza kufanya ni kuitumia lugha kuifasili dini, lakini hatuwezi kuitumia dini kuifasili lugha.
Kiswahili ni Kibantu
Vipengele vinavyotumika katika kuihalalisha nadharia inayodai kwamba Kiswahili ni Kibantu n ushahidi wa ki-Isimu, ushahidi wa ki-Historia na kuichunguza lugha ya Kiswahili katika mfumo mzima wa historia ya mgawanyiko wa kusambaa kwa lugha za ki-Bantu. Wataalamu wa nadharia hii wanahitimisha kwa kudai kwamba Kiswahili n mojawapo kati ya lugha katika jamii kubwa ya lugha za ki-Bantu.
Baadhi ya wataalamu muhimu wanaoiunga mkono nadharia hii ni Prof. Malcon Guthrie, Dkt. C. Meinholf na Dkt. C. Rohl na Prof. Clement Maganga.
Profesa Malcom Guthrie ni mtaalamu (mwanaisimu) mashuhuri kutoka Chuo Kikuu cha London, Uingereza. Alitumia miaka 20 kuchunguza uhusiano uliopo baina ya lugha za Kibantu zilizoko katika eneo lote ambalo hukaliw na wabantu. Sehemu hii ni ile ambayo inajulikan kama Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Alifanya uchunguzi wa mashina/mizizi (viini) ya maneno 22,000 kutoka lugha 200 za Kibantu. Katika uchunguzi wake alikuta mizizi (mashina) 2,300 imezagaa katika lugha mbalimbali za Kibantu na Kiswahili kikiwemo. Mashina/mizizi 500 yalilingana katika lugha zote 200. Mashina haya yalipatikana katika lugha zote za Kibantu. Mashina haya yalikuwa ya asili moja. Baadhi ya lugha hizo 200 zilizofanyiwa uchunguzi Kiswahili kilionesha kuitikia ulinganifu sawa na Kikongo kwa asilimia arubaini na nne (44%).
Katika kuchunguza ni asilimia ngapi za mashina hayo 500 yaliyomo katika kila lugha, mgawo uliojitokeza ulikuwa kama ifuatavyo:
Kiwemba kizungumzwacho Zambia -
54%
Kiluba kizungumzwacho Katanga -
51%
**Kikongo kizungumzwacho Zaire -
44%**
**Kiswahili kizungumzwacho Afrika Mashariki 44%**
Kisukuma kizungumzwacho Tanzania
41%
Kiyao kizungumzwacho Tanzania/Msumbiji -
35%
Sotho kizungumzwacho Botswana
20%
*Kirundi kizungumzwacho Burundi -
43%*
Kinyoro kizungumzwacho Uganda -
37%
Kizulu kizungumzwacho Afrika Kusini -
29%
Baada ya kupata matokeo haya, Profesa Malcom Guthrie anaiunga mkono nadharia hii ya kwamba
Kiswahili ni ki-Bantu kwa kudai kwamba:
(i) Kiswahili kilikuwepo kabla ya ujio wa wage
(ii) Anaonyesha kwamba Kiswahili kina uhusia mkubwa na lugha za Kibantu;
(iii) Mwisho anasema Kiswahili kilianzia Pwani y Afrika Mashariki.
Dkt. C. Meinholf na Dkt. C. Rohl: Wataalamu haw wanaamini kwamba:
(i) Wakati wa utawala wa Shirazi kati wa mashariki ya Afrika kulikuwa na kabila Waswahili;
(ii) Kabila hili ni dhuria ya Wazaramo w
(iii) Kwa kuwa hawa Wazaramo walikuw wamezaliwa katika harakati za kibiashara hivyo wakafuata nyayo za wazazi wao.
(iv) Lugha yao ilikuwa ya aina ya ki-Bant
(v) Kwa kuwa Wabantu ni wengi zaidi jamii ya makabila mengine, lugha yao ya ikaanza kutumika na kuenea katika maka mengine, hususan katika ukanda wa pwa Afrika Mashariki.
(vi) Baadaye, Waswahili hawa hawa wak biashara na wageni waliokuja kuvinjari Af Mashariki, hususan Waarabu, Washirazi, Wamalaysia, Wahindi na Wareno ambao t walikuwa wamefurika katika pwani hii ya Mashariki miaka kadhaa kabla.
(vii) Vifaa na majina ya vitu vya biashara v wageni hao vikaselelea na kuingizwa kati mfumo wa lugha hiyo ya Waswahili ambaBantu.
Madai ya nadharia hii yakichunguzwa, tunagundu kwamba inazingatia mitazamo miwili yaani, mtazamo wa ki-Isimu na mtazamo wa ki-Histori Kwa mantiki hii, nadharia hii inaelekea kukubalik na wataalamu wengi kuwa ndiyo sahihi kuhusu asili au historia ya Kiswahili.
Profesa C. Maganga, na uthibitisho wake kwamb Kiswahili ni ki-Bantu. Kama tulivyoona, lugha ya Kiswahili ilifanyiwa utafiti na uchambuzi na wanataaluma kadhaa kwa madhumuni ya kuiainisha kama ilikuwa yenye misingi ya ki-Bant au la. Prof. Maganga alifanya uchambuzi wa ki-Isimu na wa ki-Historia kuhusu lugha hii. Matoke ya utafiti wake wa ki-Isimu kuhusu lugha ya Kiswhili (au lugha kwa ujumla) unadhihirisha mambo mengi, mojawapo ni asili ya lugha hiyo. Amethibitisha kwamba Kiswahili ni lugha ya Kibantu; na kwa hivyo, kuthibitisha kwa ushahidi thabiti hoja ya Dkt. C. Meinholf na Dkt. C. Rohl
kama tulivyoieleza hapo juu.
(i) Ushahidi wa Kiisimu
(a) Msamiati
Matokeo ya utafiti alioufanya kuhusu msamiati w Kiswahili ulibaini kwamba 60% ya maneno yote yanayoweza kuandikwa na kutamkika katika lugh ya Kiswahili asili yake ni lugha za Kibantu, 30% n lugha ya Kiarabu na 10% ni lugha nyingine za kigeni kama vile Kiingereza, Kireno, Kijerumani, Kihindi, Kiajemi, Kifaransa, nk. Kinyume chake ni kwamba msamiati wa Kiswahili na ule wa Kibantu hautofautiani.
Mfano:
Kiswahili Kindali Kizigua Kijita Kikury
Kindendeule
Mtu Umundu Mntu Omun
Omontu Mundu
Maji Amashi Manzi Amanji
Amanche Maache
Moto Umulilo Moto Omulilo
Omoro Mwoto
(b) Tungo (Sentesi) za Kiswahili
Miundo ya tungo (sentesi) za maneno ya Kiswahili zinafanana sana na miundo ya tungo z maneno ya ki-Bantu. Sentesi za Kiswahili na za lugha za ki-Bantu zina kiima na kiarifu.
Mfano:
Lugha za Kibantu Kiima
kiarifu
Kiswahili Juma
anakula ugali.
Kizigua Juma
adya ugali.
Kisukuma Juma
alelya bugali
Kindali Juma
akulya ubbugali.
Kijita
Juma kalya ubusima.
Kindendeule Juma
ilye ughale.
(c) Ngeli za Majina
Wanataalamu wanakubaliana kuhusu ngeli za majina kwa mujibu wa:
maumbo ya nomino (umoja na wingi wa majina) pamoja; na
upatanisho wa kisarufi katika sentesi.
Kigezo cha maumbo ya majina: Kigezo hiki hufuata maumbo ya umoja na uwingi katika kuyaainisha majina. Majina yaliyo mengi katika lugha ya Kiswahili na lugha za ki-Bantu hufuata mkondo wa umoja na uwingi. Majina ya lugha ya Kiswahili na lugha za ki-Bantu yaliyo mengi yana maumbo dhahiri ya umoja na uwingi.
Mfano:
Lugha za Kibantu Umoja
Wingi
Kiswahili mtu -
watu
mtoto -
watoto
Kikurya omanto -
banto (abanto)
omona - bana (abana)
Kizigua mntu -
bhantu
mwana -
bhana
Kindali mundu -
bhandu
mwana -
bhana
Kindendeule mundu -
βhandu
mwana -
βhana
Kigezo cha upatanisho wa kisarufi katika sentesi Katika kigezo hiki tunaangalia uhusiano uliopo kati ya kiima (jina na viambishi awali vya nafsi) n vivumishi katika vitenzi vya Kiswahili na ki-Bantu Vivumishi, majina pamoja na viambishi hivyo vya vitenzi hubadilika kutokana na maumbo ya umoj na uwingi.
Mfano:
Lugha za Kibantu Umoja -
Wingi
Kiswahili Baba analima -
Baba wanalima
Kindali Utata akulima -
Abbatata bbakulima
Kikurya Tata ararema -
Batata(Tata)bararema
Kijita Tata kalima
- Batata abalima
Kindendeule Tate ilima -
Akatate βhilima
(d) Vitenzi vya Kiswahili na Kibantu
Kuna uhusiano mkubwa sana kati ya vitenzi vya Kiswahili na vile vya lugha zingine za ki-Bantu. Vipengele vinavyothibitisha uhusiano huu ni: Viambishi, mnyumbuliko, pamoja na mwanzo au mwisho wa vitenzi, kama ifuatavyo:
Viambishi: vitenzi vya lugha ya Kiswahili na vya lugha zingine za ki-Bantu hujengwa na mzizi (kiini) pamoja na viambishi vyake vya awali na vy tamati.

Mfano:
Kiswahili - analima = a – na – lim - a
Kiikuyu - arerema = a – r – rem–a
Kindali - akulima = a - ku – lim – a
1 -
2 - 3 - 4
Sherehe:
1 - Kiambishi awali kipatanishi cha nafsi.
2 - Kiambishi awali cha njeo (wakati uliopo).
3 - Mzizi/Kiini.
4 - Kiambishi tamati.
Mnyambuliko wa vitenzi: Mnyumbuliko wa vitenzi vya Kiswahili hufanana na ule wa vitenzi vya lugha za ki-Bantu.
Mfano:
Kiswahili - kucheka -
kuchekesha - kuchekelea.
Kindali - kuseka -
kusekasha - kusekelela.
Kibena - kuheka -
kuhekesha - kuhekelea.
Kinyamwezi - kuseka -
kusekasha - kusekelela.
Kikagulu - kuseka -
kusekesha - kusekelela
Mwanzo wa vitenzi: Vitenzi vyote vya Kiswahili na vile vya lugha za ki-Bantu huanza na viambis ambavyo ni viwakilishi vya nafsi, kama ifuatavyo:
Mfano:
Kiswahili - Ni-nakwenda
Kihaya - Ni-ngenda
Kiyao - N- gwenda
Kindendeule - Ni- yenda
Mwishilizo wa vitenzi: Vitenzi vya lugha za ki-Bantu na Kiswahili huishia na irabu –a.
Mfano:
Kiswahili kukimbi-a - kuwind-a -
kushuk-a
Kindali kukind-a - kubhing-a -
kukol-a
Kisukuma kupil-a - kuhwim-a -
Kutend-a
Kisunza kwihuk-a - kuhig-a
kising-a
Kindendeule kuβhutuk-a - kuhwim-a -
kuhuk-a
tafiti wa Prof. Maganga kuhusu ushahidi wa ki-Isimu wa kuthibitisha kama Kiswahili ni ki-Bantu au la ungeweza kuelezwa kimuhtasari kwa mifan mingine ifuatayo:
Mfano wa 1:
Lugha Sentesi
Kiswahili
Kipare
Kindamba
Kichaga
Kihaya
Kikaguru
Kindendeule Jongo
Jongo
Jongo
Jongo
Jongo
Jongo
Jongo anafuga
erisha
kafugha
nao he
n’afuga
kachima
ifuga mbuzi
mbuji
mene
mburu
embuzi
m’ehe
mbuhi kuk
nk
ng
ng
en
ng
ng
Katika mfano huu inaonekana kwamba mpangili wa maneno katika sentesi una ufanano kwa sababu katika kila sentesi kuna kiima na kiarifu. Katika kiima kuna nomino, yaani jina la mtenda (Jongo) na katika kiarifu kuna kitendo kinachofanyika na nomino mtendwa. Pia nafasi y viunganishi ni ile ile kwa lugha zote zilizoonyeshwa katika mfano huu.
Kuna mfano mwingine wa ufanano wa mpangilio huu.
Mfano wa 2:
Lugha Sentesi
Kiswahili
Kihaya
Kisukuma
Kinyaturu
Kipare
Kizigua Sitamkuta kesho
Timushangemu nyenkya
Natusanga intondo
Tumuhanga fadyu
Nesikemkiche yavo
Sirambila luvi
Katika sentensi hizo mpangilio wa maneno una ufanano kwa sababu kila sentensi ina kiima na kiarifu chenye kitenzi na kielezi. Pia kiambishi ch nafsi cha nomino ya mtenda kinajitokeza mwanzoni mwa neno la kwanza la kila sentesi.
Si tamkuta; Ti mushangemu; Na tusanga;
Tu muhanga; Nesikamkiche;
Si tambila.
Viambishi hivyo vya nafsi ya mtenda pia vinaonyesha hali ya ukanushi katka kila sentesi n nafasi yake ni ile ile kwa kila sentesi.
Viambishi vya urejeshi navyo vinajitokeza katika kitenzi cha kila sentesi.
Viambishi {m}, {m}, {ti}, {tu} sita m kuta,
ti mushangemu, natusanga, tumuhanga, nesika m kiche, na sita m bwila ni vya urejeshi; vinawakilisha nomino mtendwa.
Kwa hivyo, hali hii inadhihirisha kwamba miundo ya sentensi hizi inafanana na vitenzi vyake vina tabia mbalimbali, kama vile:
(i) kubeba viambishi vya nafsi, mtenda na mtendwa,
(ii) kuonyeshga hali ya ukanushi njeo za wakati na kitendo kinachofanyika.
Mfano wa 3:
Lugha
Kiswahili
Kizigua
Kihaya
Kisukuma
Kinyaturu
Kipare
Kindendeule Akija mwam
Akeza umug
Kalaija omug
Ulu nahali an
Newaja mwe
Ekiza umti a
Anda ahikite angobhekera
Katika sentesi hizo inaonekana kwamba sentesi zote zinafanana kimpangilio. Pia maneno yake yanakubali uambishaji, kwa mfano:
(i) Katika maneno ya mwanzo:
akija, akeza. kalaija, akuja, newaja, ekiza, zilizopigiwa vistari ni viambishi vya nafsi vinawakilisha dhana ya mtenda.
(ii) Vivyo hivyo katika maneno:
anifuate, ampondele, anitimile, ang’nge, a angobhekeraye, viambishi vilivyoko katika vya sentesi hizo vinawakilisha nafsi za w
(iii) Pia vitenzi vya sentesi hizo vina tabia ya k virejeshi vya nafsi kama ilivyo katika, m w omugambile, naha li, m b wele na um ti, vina njeo na hali ya uyakinifu- hali inayoonyes ufanano wa maumbo ya maneno.
(iv) Licha ya kuwa na mpangilio unaofanana n lugha nyingine za kibantu, kwa mfano, kat mifano tuliyoiona hapo juu, baadhi ya ma yanafanana: tazama maneno:
kafugha (Kindamba); nafuga (Kihaya);
nifuga (Kindendeule); anafuga (Kiswahili
Pia maneno:
nkuku (Kipare); nguku (Kindamba);
nguku (Kichaga); enkoko
(Kihaya);
ng’uku (Kikaguru); nguku(Kindendeule);
nguku (Kindendeule)
Katika mfano wa 3, maneno yafuatayo yana ufanano:
Akeza (Kizigua); kalaija (Kihaya);
alize (Kisukuma),
newaja (Kinyaturu); ekiza (Kipare);
anda ahikite,... (Kindendeule);
akija, (Kiswahili.)
Pia maneno;
umugambe (Kizigua); omugambile
(Kihaya); unongeraye (Kindendeule); na mwambie (Kiswahili).
Ufanano huu wa msamiati, maumbo ya maneno pamoja na wa mpangilio wa maneno katika sentesi, vyote vinathibistisha kwamba lugha ya Kiswahili ni ya kibantu kama zilivyo nyingi nyinginezo.
(ii) Ushahidi wa Kihistoria Kwamba Kiswahili ni Kibantu
Baada ya kuangalia ushahidi wa kiisimu kuhusu asili ya Kiswahili, katika sehemu hii Maganga (1997) aliendelea kuchambua ushahidi wa Kihistoria unaothibitisha kuwa lugha ya Kiswahili ilizungumzwa katika upwa wa Afrika Mashariki hata kabla ya ujio wa wageni kama vile Waarabu na Wazungu. Ushahidi huu ulitolewa na wageni mbalimbali waliofika hapa Afrika Mashariki. Wot wanathibitisha kuwa lugha ya Kiswahili ilizungumzwa hapa Afrika Mashariki kabla ya uji wa wageni.
(a) Ugunduzi wa Ali-Idris (1100-1166)
Ugunduzi huu yasemekana ulifanywa huko Sicily yapata mwaka 1100-1166. Kwenye mahakama y mfalme Roger II. Licha ya kufahamika kuwa Kiswahili, kilipata kuandikwa kabla ya 10BK. Ali-Idris alikuwa wa kwanza kugundua jina la zaman la Zanzibar kuwa ni Unguja. Katika maelezo yake anaandika pia majina kama vile kikombe, mkono wa tembo, muriani, na kisukari, ambayo ni ya ndi mbalimbali zilizokuwa zikipatikana huko.
(b) Ushahidi wa Marco Polo
Huyu ni mzungu ambaye alijishughulisha sana n masuala mbalimbali ya kijiografia na alisafiri sehemu nyingi duniani. Marco Polo aliandika hivi
“Zanzibari ni kisiwa kizuri ambacho kina ukubwa wa mzunguko wa maili 200. Watu wote wanaabudu (Mungu), wana Mfalme na wanatumi lugha yao, na hawalipi kodi (ushuru) kwa mtu.”
Safari za Marco Polo 1958:301
Marco Polo anasemekana aliandika pia kitabu ch jiografia ambacho hakikupata kuchapishwa lakini sehemu zake zimepata kufasiriwa kwa Kirusi na Kifaransa. Mfano mmojawapo ni huu unaofuata:
“Katika visiwa vya Sjawaga vilivyoshughulikiwa katika sura hii, ni kile kisiwa cha Andjaba ambacho mji wake mkuu unaitwa katika lugha ya kwao. Zanguabar/Ungudya, na wakazi wake, japokuwa ni mchanganyiko, kwa sasa wengi wao ni Waislam…chakula chao kikuu kikiwa ndizi. Kun aina tano ambazo zinajulikana kama kundi, fili, ambazo uzito wake waweza kuwa wakia 12, Omani, Marijani, Sukari....”
Maelezo haya ya Marco Polo yanathibitisha mambo ya msingi kuhusu wakazi wa Pwani ya Afrika ya Mashariki na lugha yao; mintarafu ya dini, chakula na utamaduni wao kwa ujumla.
(c) Ushahidi wa Al-Masudi (915 BK)
Katika moja ya maandiko yake, Al-Masudi anazungumzia juu ya wakazi wa mwambao ambao walijulikana kwa jina la “wazanji”. Kwa dhana hii, neno Zanzibar linatokana na Zenzibar yaani “Pwani ya Zenji”. Katika maelezo yake Al-Masudi anaonyesha kwamba Wazenji walikuwa
“Watawala Wakilimi” ambao waliaminiwa kuwa walitawala kwa nguvu za Mungu. Kuna maelezo kuwa huenda neno “wakilimi” lina maana ya “wafalme”. Al-Masudi alisisitiza katika maelezo yake kuwa Wazenji walisema lugha kwa ufasaha na walikuwa na viongozi waliowahutubia kwa lugha yao. Kutokana na neno “zenji” kuna uwezekano kuwa kabla ya majilio ya Waarabu, Kiswahili kiliitwa “Kiazania” au “Kizanji” na wage waliofika pwani.
(d) Ushahidi wa Ki- Historia wa Mji wa Kilwa
Kimsingi habari zinazoeleza historia ya mji wa Kilwa katika karne ya 10-16BK zinataja majina ya utani kama vile: mkoma watu, nguo nyingi , nk. ambayo walipewa Masultani wa kwanza wa Kilw Ali Ibn Hussein na mwanae Mohamedi Ibn Ali. Kutokana na habari hizi huenda lugha ya Kiswahi ilishaanza kusemwa mnamo karne ya 10 au ya 1 BK. Maelezo ya kihistoria yanaeleza juu ya Sulta aliyeitwa Talt Ibin Al Husaini ambaye alipewa jin la utani “ Hasha Hazifiki”.
(e) Utenzi wa Fumo Liyongo (13 BK) kama Ushahidi
Shairi la zamani kabisa lililopata kuandikwa la Kiswahili, linalojulikana ni lile la Utenzi wa Fumo Liyongo . Utenzi huu inasemekana uliandikwa karne ya 13BK. Kuweko kwa shairi hili kunadhihirisha kuwako kwa lugha ya Kiswahili kabla ya karne hiyo, na kwa hivyo, huenda Kiswahili kilianza kutumika kabla ya karne ya 10BK. Baadhi ya beti za utenzi wa Fumo Liyongo ni hizi zifuatazo:
Ubeti 6: Liyongo Kitamkali,
Akabalighi vijali
Akawa mtu wa kweli
Na hiba huongeya.
Ubeti 7: Kilimo kama mtukufu
Mpana sana mrefu
Majimboni yu maarufu
Watu huja kwangaliya.
Ubeti 10: Sultani pate Bwana
Papo nae akanena
Wagala mumemwona
Liyongo kiwatokeya.
(Kutoka E.A. Swahili Committee 1973)
Lugha hii ndio mfano wa lugha iliyokuwa ikitumik kunako karne ya 13BK. Ni wazi kuwa lugha hiyo ilianza kusemwa mapema kabla ya muda huo. Hoja za kihistoria inaelezea historia ya lugha ya Kiswahili toka karne ya 10BK hadi karne ya 18BK Kutokana na ushahidi huu ni dhahiri kuwa asili ya lugha ya Kiswahili ni Wabantu wa Afrika ya Mashariki.

Maoni