NEEMA YAISHUKIA MBAO FC, YAPATA UDHAMINI MNONO

Mafanikio yao katika msimu wa kwanza katika ligi kuu Tanzania bara yameshusha neema kwa klabu ya Mbao FC ya jijini Mwanza baada ya kupata udhamini mnono toka kampuni ya Uuzaji wa magari makubwa na matela ya mizigo ya GF Trucks and equipment limited ya jijini Dar es Salaam.

Mkataba wa Makubaliano kati ya klabu hiyo iliyofika fainali ya kombe la FA msimu uliopita na kampuni hiyo yameafikiwa katika makao katika makao makuu ya kampuni hiyo yaliyoko vingunguti jijini Dar es salaam na kusainiwa katika ofisi za shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF Leo baina ya Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo Bwana Imran Karmali na Mwenyekiti wa klabu ya Mbao Fc Zephani Njashi huku kila mmoja akiusifu mkataba huo wa kihistoria kwani unaelekea kukuza maendeleo ya mpira nchini Tanzania na pia unahamasisha soko kubwa kwa GF Trucks and Equipment huausani maeneo ya kanda ya Ziwa.

"Tuna matumaini wakati huu wa ufadhili wetu Mbao Fc itaendelea kufanya vizuri, sio tu Mbao Fc lakini Pia mpira wa Tanzania kwa ujumla kwa sababu kwa njia ya mchezo huu tunaamini tunatengeneza ajira nyingi zaidi” Alisema Bwana Imran Karmali.

Mkataba huu wa Udhamini huu kampuni ya  GF Trucks and Equipment limited kwa Mbao FC unakadiriwa kuwa ni wa shilingi milioni 140 kwa mwaka ambao utajumuisha na basi la timu kwa misimu ya 2017/2018 na 2018/2019 na umeanza rasmi Agosti 25 na utaifanya nembo ya GF Trucks and Equipment kuonekana kwenye jezi za klabu hiyo pamoja na basi lao kwa misimu hiyo miwi.

Maoni