OMOG ATAMANI KALENDA YA FIFA ISINGEKUWEPO SIMBA IENDELEZE VIPIGO



Kocha Joseph Omoga anaonyesha kutofurahishwa na kusimama kwa Ligi Kuu Bara.

Ligi Kuu Bara imesimama kutokana na kalenda ya Fifa ikiwa ni baada ya timu kucheza mechi moja tu.

Omog amewaambia wasaidizi wake, angependa muendelezo kwa kuwa kikosi chake kilikuwa kimeshapata moto.

Simba ilianza ligi kwa kishindo ikiishindilia Ruvu Shooting mabao 7-0 katika mechi ya kwnaza.

Baada ya hapo, timu zimekwenda mapumziko na Omog anaona watakuwa kama wanaanza upya kuitafuta kasi waliyoanza nayo.

"Kocha alipenda iwe muendelezo, kama tumeanza ligi tumeanza kuliko kuanza halafu mechi inayofuatia tunasimama. Lakini anaendelea kulifanyia kazi hilo," kilieleza chanzo.

"Unajua anachotaka kocha ni ushindi na uwe wa mabao mengi, lakini haiwezi kuwa rahisi kwa kila mechi. Kwa sasa anaendelea kulifanyia kazini hilo tukiwa mazoezini."

Maoni