Ripoti ya Mkemia wa Serikali kuhusu sampuli ya mkojo wa Agness Masogange Yapokelewa Mahakamani....Pingamizi Latupwa

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo August 28, 2017 imepokea taarifa ya Mkemia kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali iliyoonesha kuwa sampuli ya mkojo wa Agnes Gerald maarufu kama Masogange una chembechembe za dawa za kulevya.
Taarifa hiyo imepokelewa baada Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri kutoa uamuzi wake ambapo amesema Mahakama imepokea taarifa hiyo na pingamizi la utetezi limetupiliwa mbali.
Pingamizi la upande wa utetezi ni kwamba fomu zilizopelekwa kwa Mkemia Mkuu hazikufuata sheria.
Hakimu Mashauri amesema Mkemia huyo Elia Mulima ambaye ni Shahidi wa kwanza ana haki ya kuandaa ripoti, kupima sampuli na kutoa ripoti Mahakamani.
Kuhusu hoja ya kuwasilishwa maombi ya kupimwa mkojo Masogange, Hakimu amesema ni wazi Polisi walipeleka maombi kwa Mkemia na mshtakiwa alienda akiwa chini ya askari wawili, ambapo walipatiwa kontena kwa ajili ya kuweka sampuli ya mkojo wa Masogange.

Maoni