Roma Mkatoliki avunja rekodi

Msanii Roma Mkatoliki ambaye sasa yupo nchini Zimbabwe na anayefanya vizuri na wimbo wake mpya Zimbabwe amevunja rekodi yake mwenyewe baada ya wimbo wake mpya kufanya vizuri zaidi katika mtandao wa You Tube.
Siku ya Alhamisi tarehe 10 Agosti 2017 Roma Mkatoliki alipandisha kwenye mtandao wa You Tube video ya wimbo wake mpya ambao umeonekana kuwagusa watu wengi kutokana na ujumbe wake na mashairi ambayo yapo kwenye wimbo huo, hali ambayo imefanya video hiyo kutazamwa na watu wengi zaidi ndani ya muda mfupi mpaka kufikia hatua ya kuwa video namba moja inayofanya vizuri kwenye mtandao huo kwa takribani siku zote tatu toka imetoka.
Ndani ya masaa 75 Video mpya wa Roma Mkatoliki imetezamwa na zaidi ya watu laki sita na kuvunja rekodi kwa video kadhaa ambazo Roma Mkatoliki amewahi kuziweka kwenye mtandao huo kwa mfano, mwaka mmoja uliopita Roma Mkatoliki alitoa wimbo unaoitwa 'Kaa Tayari' aliomshirikisha Jos Mtambo na Darassa video yake mpaka sasa imetazamwa na watu laki tatu na kitu.
Mwanzoni mwa mwaka huu tarehe 15 Januari, Roma Mkatoliki aliachia video ya wimbo wa kushirikiana unaoitwa 'Usimsahau Mchizi' akiwa na Moni Centrozone video hiyo mpaka sasa imetazamwa na zaidi ya watu laki tatu na kitu hii ndiyo ilikuwa kazi ya mwisho kwa Roma Mkatoliki kwani baada ya hapo alipatwa na matatizo ya kutekwa na aliporejea aliendelea kuuguza majeraha yake na kujiweza sawa mpaka alipokuja kudondosha wimbo huu mpya ambao unaonekana kukata kiu ya mashabiki wengi wa muziki na mashabiki wa Roma Mkatoliki.
Mpaka sasa 'Zimbambwe' yake Roma Mkatoliki imevunja rekodi kwa kuwa na watazamaji wengi zaidi ndani ya muda mfupi kwa ngoma za Roma, ikumbukwe kuwa kwa wasanii wa Hip hop video ambayo iliwahi kupokelewa kwa speed hii ni 'Muziki' ya Darassa ambayo ndani ya wiki mbili iliweza kufikisha watazamaji milioni moja na kuwa namba tano katika video zinazo 'Trend' kwa kipindi hicho, Video nyingine ambayo imewahi kuwa na kasi hiyo kwa upande wa wasanii wa Hip hop ni 'Dume Suruali' ya Mwana FA akimshirikisha Vanessa Mdee.

Maoni