Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imezifuta timu mbili kutoka daraja la pili.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imezifuta timu mbili kutoka daraja la pili kwa kushindwa kukamilisha usajili wa vilabu vyao katika kuelekea michuano ya Ligii kwa msimu wa mwaka 2017/2018.
Hayo yamebainishwa na taarifa iliyotolewa na Afisa habari wa (TFF), Alfred Lucas na kusema timu hizo zimeshindwa kujisajili, kuingiza majina ya wachezaji pamoja na kuingiza viongozi wa benchi la ufundi kwenye mfumo wa mtandao 'Transfer Matching System' (TMS) ni za Ligi Daraja la Pili (SDL) ambazo ni Pepsi ya Arusha na Bulyanhulu ya Shinyanga.

Maoni