SIJAWAHI ONA UGUMU WOWOTE AU KUWAZA NIRUDI TANZANIA, ABDI BANDA.

Beki wa zamani wa Simba Abdi Hassan Banda ni mmoja kati wachezaji waliyoitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars kitakachocheza game ya kirafiki dhidi ya Botswana September 2 2017 uwanja waUhuru, Abdi Banda Msimu huu anacheza Baroka FCya Afrika Kusini.
Abdi Banda anaichezea Baroka FC inayoshiriki Ligi Kuu Afrika Kusini na hivi karibu aliifungia goli muhimu kwenye timu yake ya Baroka dhidi ya Orlando Pirates katika sare ya 1-1,Banda alifunga goli hilo kwa kichwa.
 “Maisha ya kule sijaona ugumu wowote au kupata mawazo ya kusema nirudi nyumbani au nirudi Tanzania, ilikuwa ni rahisi kupata nafasi ya kucheza maana kule hawaangalia kuwa Banda proffesional wanachoangalia uwezo wako na ukiwa fiti mazoezini” Alisema Abdi Banda. 
Ndugu Msomaji wa Nijuzehabari Blog Banda alifunguka hayo baada ya kumaliza mazoezi kwenye Uwanja wa Uhuru yanapofanyika kwa siku 4, ambapo kesho Ijumaa watamaliza, na Jumamosi kuwavaa Wabotswana pale Uhuru Majira ya saa 16:00 Jioni.

Maoni