SIMBA YAKAMILISHA USAJILI WAKE NA KIFAA TOKA GHANA.

Mshambuliaji Nicolas Agyei jana ametambulishwa rasmi katika klabu yake mpya ya Simba.
Agyei ametambulishwa makao makuu ya klabu ya Simba baada ya kuwasili nchini juzi usiku.
Raia huyo wa Ghana amekuwa ndiye mchezaji wa mwisho kujiunga wakati wa usajili.
Msemaji wa Simba, Haji Manara ndiye aliyemtambulisha Agyei mbele ya baadhi ya waandishi wa habari na baadhi ya wanachama wa Simba waliokuwa klabuni hapo.
Pamoja na Mghana huyo, wengine waliotambulishwa klabu hapo ni Haruna Niyonzima, Emmanuel Okwi na wenyeji wawili, Method Mwanjale na Mohamed Hussein Zimbwe.

Maoni