STARTIMES YAONGEZA NGUVU ALL STAR, MECHI INAPIGWA JUMAMOSI


Wadhamini wakuu wa ligi ya kikapu ya RBA, kampuni ya StarMedia Tanzania Limited sasa wameleta mechi ya All Star ambayo itashirikisha wachezaji vinara katika ligi hiyo. Mechi ya All Star inatarajiwa kuchezwa siku ya Jumamosi tarehe 2 mwezi wa tisa.

Baada ya kuanza kwa hatua ya robo fainali (playoffs), wapenzi wa mpira wa kikapu jijini Dar es Salaam na Tanzania Kwa ujumla watapata nafasi ya kushuhudia wachezaji vinara wa ligi hiyo wakiwapatia burudani Stahiki kupitia mchezo wa All Star. 

Maoni