Twamtaka mwenyekiti wa IEBC atangaze matokeo na kumtangaza Odinga

Twamtaka mwenyekiti wa IEBC atangaze matokeo na kumtangaza Odinga na Kalonzo rais mteule na naibu rais mteule wa Kenya mara moja," amesema Bw Mudavadi.
Muungano wa upinzani Kenya Alhamisi uliendelea kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais yanayotangazwa na tume hiyo kwenye mtandao wake.
Viongozi wa muungano wa National Super Alliance wamesema walikutana na wakuu wa Tume ya Uchaguzi Kenya na kuwasilisha rasmi malalamiko yao kupitia barua.
Ajenti mkuu wa upinzani Musalia Mudavadi, ambaye ni naibu waziri mkuu wa zamani, amesema upinzani umepata maelezo zaidi kwamba matokeo ya uchaguzi yalivurugwa baada ya kudukuliwa kwa mitambo ya IEBC.
Wakuu wa IEBC wamekanusha kwamba mitambo ilidukuliwa. Mwenyekiti Wafula Chebukati amesema kulikuwa na jaribio la kudukua mitambo hiyo, lakini halikufanikiwa.
Bw Mudavadi amedai mgombea wa upinzani Raila Odinga ndiye aliyeshinda uchaguzi huo.

Maoni