UBELGIJI NOMA, YAIFUMUA GIBRALTAR 9-0, LUKAKU APIGA TATU

Mashujaa wa hat-trick, Romelu Lukaku na Thomas Meunier wakipongezana baada ya kazi nzuri kwenye ushindi wa 9-0 wa Ubelgiji dhidi ya Gibraltar usiku wa jana katika mchezo wa Kundi H kufuzu Kombe la Dunia Uwanja wa Maurice Dufrasne mjini Liege, Ubelgiji. Lukaku alifunga dakika za 21, 38 na 84 kwa penalti, wakati na Meunier alifunga dakika za 18, 60 na 67 wakati mabao mengine ya Ubelgiji yamefungwa na Deren Ibrahim aliyejifunga dakika ya 15, Axel Witsel dakika ya 27 na Eden Hazard dakika ya 45

Maoni