UHARAMU WA MWANAMKE KUJIPULIZIA MANUKATO

Jambo hili la wanawake kujipulizia _MANUKATO AU KUJIFUKIZA UDI_ limeenea mno katika majumba yetu pamoja na kuwapo onyo kali kutoka kwa Mtume swalla llahu alleh wasalaam:
ﺃﻳﻤﺎ ﺍﻣﺮﺃﺓ ﺍﺳﺘﻌﻄﻓﻤﺮّﺕ ﺑﻘﻮﻡ
ﻟﻴﺠﺪﻭﺍ ﺭﻳﺤﻬﺎ ﻓﻬﻲ ﺯﺍﻧﻴﺔ ﺭﻭﺍﻩ ﺍﻹﻣﺎﻡ ﺃﺣﻤﺪ ﻭﻏﻴﺮ
*_“Mwanamke yoyote aliyejitia uturi [manukato] kisha akajipitisha mbele ya watu ili waipate harufu yake, basi mwanamke huyo ni mzinifu.”_*
_Mghafala, dharau na hali ya kutojali waliokuwa nayo baadhi ya wanawake huwafanya kulipuuza jambo hili na kutotilia maanani ipasavyo._
_Lakini sharia ya kiislamu imesisitiza vikali kwamba mwanamke yeyote mwenye kujitia manukato kisha anatoka nje japo kama atakuwa amekwenda msikitini ni lazima aoge josho la janaba_
_Amesema Mtume swalla llahu alleh wasalaam: “Mwanamke yoyote aliyejitia manukato kisha akatoka kwenda msikitini ili [wanaume] waipate ile harufu yake hatokubaliwa sala yake mpaka atakapooga josho lake la janaba.”_
_Utawaona wanawake wa zama zetu wakishindana kwa manukato mablimbali wakati wa kwenda kwenye sherehe na wakati mwengine hutumia manukato yenye harufu kali wakiwa masokoni, au kwenye usafiri au kwenye jamii zenye kuchanganyika wanawake na wanaume pamoja, na ahata misikitini kwenye Ramadhani._
_Inafaa ieleweke kuwa sharia imeweka wazi kwamba, manukato ya mwanamke yanatakiwa yawe yale yenye kudhihirisha rangi na kupotea au kujificha harufu yake_
*Au kama ni MANUKATO ya kunukia basi ajifukize ndani akiwa na mume wake*

Maoni