Vibaka wa mitandaoni almanusra wawaingize Cr7 na Romelu Lukaku katika mzozo

Teknolojia imekuwa kubwa siku za usoni na watu wanatumia mitandao ya kijamii kurahisisha mawasiliano yao, lakini mitandao hiyo hiyo wapo wanaoitumia vibaya na kuleta machafuko.

Wahalifu wa mitandao walifanikiwa kuiba account ya mshambuliaji wa Manchester United Romelu Lukaku, hawakuishia hapo tu bali walienda mbali zaidi na kufanya jambo linaloweza kuleta ugomvi kati ya Lukaku na Cristiano Ronaldo.

Baada ya tukio la Ronaldo kumsukuma muamuzi katika mchezo wa El Classico na kupewa adhabu ya kukaa nje michezo mitano, Ronaldo aliandika mtandaoni kutovutiwa kwakwe na maamuzi ya tukio hilo.

Sasa wakati Cristiano akijitetea kupitia Instagram account yake kati ya watoa maoni wa tukio hilo mmoja wapo alikuwa ni Lukaku ambaye aliandika Lioneil Messi ni bora kuliko Cristiano Ronaldo.


Baada ya muda comment hiyo ilifutwa lakini watu walishaiona, ilibainika kwamba hakuwa Lukaku aliyeandika hivyo bali account yake iliibiwa japokuwa hadi sasa Lukaku mwenyewe hajaongea lolote kuhusiana na tukio hilo.

Maoni