WAZAZI WADAIWA KUMUUA MTOTO KISHA KUMFUKIA KORONGONI MBEYA.

Jeshi la polisi mkoani mbeya linawashikiria wanafamilia watatu akiwemo baba na mkewe kwa tuhuma za mauaji ya mtoto wao wa miaka 13 Farao Wilison na kumzika korongoni Iwindi mkoani mbeya
Akizungumza Naibu kamishina wa polisi kamanda wa polisi mkoani Mbeya Mohamed Mpinga amesema wanawashikiria ndugu watatu akiwemo baba ,mama mzazi pamoja na baba mdogo wa marehemu.
Kamanda amesema marehemu amekutwa akiwa na majeraha kadhaa katika mwili wake huku akikutwa na kamba shingoni,kuvunjika kwa mbavu mbili za kushoto,kichwani alikuwa na majeraha pamoja na mguu wake kuvunjika huku ikidaiwa awali kulikuwa na ugomvi wa mtoto na baba lakini uliishi na kwamba uchunguzi bado unaendelea.
Kamanda amesema licha ya uchunguzi kuendelea kuwashikilia watuhumiwa hao bila shaka huenda wazazi au ndugu wakaribu wameshiriki katika mauaji hayo kwani wazazi licha ya mtoto wao kupotea july 31 mwaka huu hawakutoa taarifa sehemu husika .

Maoni