Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba ameagiza mamlaka zinazohusika kutowawekea vikwazo WAKULIMA

Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba ameagiza mamlaka zinazohusika kutowawekea vikwazo WAKULIMA wanapotaka kusafirisha mazao yao ndani ya nchi.
Dkt. Tizeba amesema wakulima waliokamilisha vigezo vya usafirishaji hakuna namna yoyote ya kuwazuia.
Pia amewataka wakulima kujiwekea akiba ya chakula, kuliko kuuza chote wakitegemea cha msaada kutoka serikalini pindi njaa inapojiri.
Kauli Mbiu ya Mwaka huu ni "Zalisha kwa Tija Mazao ya Bidhaa za Kilimo, Mifugo na Uvuvi ili Kufikia Uchumi wa Kati"

Maoni