Zambia kuwa mwenyeji wa mkutano wa kimataifa kuhusu elimu ya wasichana barani Afrika Zambia itaandaa mkutano wa kwanza wa kimataifa kuhusu elimu ya wasichana wa Afrika, ambao unatarajiwa kuhudhuriwa na wajumbe 500, wakiwemo wake watatu wa viongozi wa Malawi, Mali na Uganda. Mkutano huo wa siku tatu unaoanza leo ulioandaliwa na Baraza la wataalamu wa elimu ya wanawake wa Afrika kwa kushirikiana na wizara ya elimu ya Zambia, unalenga kuweka mkakati na kutoa fursa za kuhimiza uongozi wa vijana na ushirika wao kwenye mazungumzo ya elimu ya kikanda, kibara na kimataifa kuhusu usawa wa kijinsia.

Zambia kuwa mwenyeji wa mkutano wa kimataifa kuhusu elimu ya wasichana barani Afrika
Zambia itaandaa mkutano wa kwanza wa kimataifa kuhusu elimu ya wasichana wa Afrika, ambao unatarajiwa kuhudhuriwa na wajumbe 500, wakiwemo wake watatu wa viongozi wa Malawi, Mali na Uganda. Mkutano huo wa siku tatu unaoanza leo ulioandaliwa na Baraza la wataalamu wa elimu ya wanawake wa Afrika kwa kushirikiana na wizara ya elimu ya Zambia, unalenga kuweka mkakati na kutoa fursa za kuhimiza uongozi wa vijana na ushirika wao kwenye mazungumzo ya elimu ya kikanda, kibara na kimataifa kuhusu usawa wa kijinsia.

Maoni