FAIDA ZA KULA SAMAKI

1. Samaki (Husausan Saladini, Tuna, Salmoni nk) wana kiasi kikubwa cha virutubisho mafuta viitwavyo Omega-3-Fatty Acids –Â Omega-3 fatty acids ni mafuta muhimu sana kwa afya zetu kwa ujumla. Husaidia kudhibiti na kushusha presha na kiasi cha rehemu mwilini (Cholesterol) na husaidia kupunguza uvimbe. Pia husaidia sana kulinda miili yetu na kukinga seli zetu dhidi ya kemikali hatari mwilini ziitwazo “free radicals”. Kinga hii ni muhimu sana kwetu na husaidia uhai wa seli na miili yetu
2. Samaki wana kiasi kikubwa cha protini – Kama unahitaji protini nyingi basi kula samaki wa kutosha
3. Samaki wana kiasi kikubwa cha madini na vitamini – Kama unahitaji vitamini na madini mengi basi kula samaki wa kutosha pia. Wana vitamini/madini ya calcium (Husaidia kujenga meno na mifupa imara),
phosphorus (Husaidia kujenga meno na mifupa imara), vitamin D (Husaidia Calcium kuweza kuingia mwilini na kuimarisha mifupa. Upungufu wa Vitamini D hupelekea mtu kuwa na matege), vitamin B2 (Husaidia kuimarisha kinga ya mwili na nywele, ngozi, mifupa na meno), iron , zinc (Husaidia kuboresha kinga ya mwili), iodine  ,
magnesium (Husaidia kusinyaa na kufanya kazi kwa misuli) na potassium (Husaidia utengenezaji wa protini na kujengwa kwa misuli).
USHAURI
Wataalam wa afya tunakushauri kula zaidi samaki kuliko nyama ya ng’ombe, mbuzi na kondoo. Kula samaki wa kutosha na usiache muda mrefu bila kula samaki. samaki ni nyama nyeupe, haina matatizo sana kama nyama nyekundu za ng’ombe, mbuzi na kondoo. Usitumie mafuta mengi kuandaa samaki, na kama ukiweza wachome au wachemshe ili kuepuka kula mafuta mengi.
Kula sana samaki kwa afya yako.
Share this:
WhatsApp Facebook Telegram
Twitter LinkedIn

Maoni