Hizi ndizo faida za kunywa kahawa -

Wataalamu wanaorodhesha faida zinazohusiana na matumizi ya kahawa. Mojawapo ni kwamba, inamfanya mtu awe nadhifu ndani ya kipindi kifupi.
Hiyo, inaelezwa kuwa ni hali inayoendana na akili kuchangamka ndani ya muda mfupi, ambao ni wastani wa dakika 45 tu.
Kwa mujibu wa watafiti kutoka Chuo Kikuu cha John Hopkins, ni kwamba kumbukumbu za mnywaji zinakuwa juu na ndani ya saa 24.
Utafiti linganishi kutoka kwa watu wawili, aliyetumia kahawa na asiyetumia katika kipindi cha siku mbili, tofauti yao ilionekana ikiwa bora kwa kumbukumbu za watumia kahawa.
Mmoja wa watu wanaotajwa kuwa ‘walevi’ wa kahawa, David Lynch anasifu matumizi ya kahawa kupitia kauli:"Hata kahawa mbaya ni nzuri kuliko kuikosa kabisa."
Faida ya pili ni kwamba, mtu anapotumia kahawa anawekwa mbali na ugonjwa wa mwili kutetemeka (Parkinson) na hata inapotokea dalili ya mtu anaumwa, anashuriwa aendeleze kunywa kahawa.
Watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Havard nchini Marekani, mwaka 2015 walikuwa na hoja kuwa unywaji kahawa vikombe kati ya vinne au vitano kwa siku, inasaidia kuondoa maradhi ya kutetemeka.
Pia kulikuwapo utafiti mwingine unaofanana na huo mwaka 2012, kuhusiana na Caffeine.
Jingine ni kwamba, inaongeza kasi ya mwili kufanya kazi, hali inayojionyesha hata kwa wanariadha. Inashauriwa kwamba, kabla ya mtu kuanza kazi, anatakiwa apate walau kati ya vikombe viwili hadi vitatu.
Chuo Kikuu cha Harvard, Marekani nacho kimefanya utafiti na kugundua kwamba kahawa inaondoa uwezekano wa mtu kupata kirahisi kisukari aina ya pili, inayotokana na mfumo binafsi wa maisha.
Tano, ni kwamba inaondoa uchovu mwilini hasa nyakati za asubuhi, kama Wataalam wa Kituo cha Utafiti wa Jeshi la Uingereza wanavyofafanua uzoefu wao kutoka kwa askari wao.
Sababu nyingine, caffeine ni tiba ya aina yake, ikichanganywa na dawa za maumivu, inatajwa kuwa dawa ya kudumu na inayotegemewa kutibu maumivu ya kichwa
Unaweza kuamini caffeine, inayopatikana sana kwenye kahawa, inatengeneza nywele nzuri? Watafiti wa Kijerumani wameligundua hilo kwa matumizi yake.
Aidha, katika suala la kansa ya mdomo na koo, Chama cha Wenye Kansa cha Marekani, kinasema kuwa matumizi ya kahawa na vyanzo vingine vya caffeine kila siku, inasaidia kupunguza maradhi hayo.
Ni utafiti uliofanyika kwa kuhusuisha jumla ya watu milioni moja katika kipindi cha miaka 26 mfululizo na ndipo walipogundua kuwepo uhusiano huo.
“Hatuwashauri watu wote kunywa vikombe vinne vya kahawa mkwa siku. Hii ni habari njema kidogo kwetu sisi tunaotumia kahawa kidogo,” infafanua ripoti ya utafiti.
L Makala hii imeandaliwa kwa kutumia vyanzo mbalimbali.

Maoni