Kwa miaka 29 Palace hawajawahi kuwafunga United OT katika Epl, leo wataweza?

Michezo 16 iliyopita ambayo Crystal Palace walikutana na Manchester United hawajawahi kupata ushindi hata mara moja, Palace walifanikiwa kutoa suluhu 3 huku michezo 13 iliyobaki wakipoteza.
Mara ya mwisho Palace wanaifunga United ilikuwa ni miaka karibia 6 iliyopita wakati wa mchezo robo fainali ya ligi mwaka 2011 ambapo Palace waliifunga United mabao 2 kwa 1.
Lakini katika mchezo wa ligi kuu Uingereza Crystal Palace waliifunga Manchester United mwaka 1988 na hii leo inaweza kuwa nafasi kwa mwewe hao kufanya walichokifanha miaka 29 iliyopita.
Lakini haitakuwa rahisi kwa Palace kuisimamisha Manchester United ambao wanahitaji alama 3 ili kufikia rekodi yao ya mwaka 1999 na ya 2001 kupata alama 19 katika michezo 7 ya mwanzo.
Tishio zaidi kwa Palace atakuwa Romelu Lukaku ambaye rekodi zinaonesha yeye peke yake katika michezo 21 ya ligi amefunga mabao 19 idadi ambayo ni kubwa kuliko magoli waliyogunga timu nzima ya Crystal Palace katika michezo hiyo.
Hadi sasa Palace ndio timu pekee Epl ambayo haina alama hata moja katika michezo yao 6, rekodi ambayo iliwekwa na Portsmouth msimu wa 2009/2010 na hii inawaweka kwenye nafasi kubwa kuendelea kukosa point hii leo.
Michezo mingine hii leo Huddersfield watakuwa nyumbani kuikaribisha Tottenham, Stoke City dhidi ya Southampton, Westham dhidi ya Swansea City na Afc Bournamouth wataikaribisha Leicester City.

CHANZO: SHAFII DAUD

Maoni